Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, August 27, 2013

BOTI YAZAMA ZIWA VICTORIA WATANO WAHOFIWA KUFA MAJI.


Watu watano kati ya nane waliokuwa wakisafiri na boti kutoka kijiji cha BUKUMBO wilayani Sengerema wanahofiwa kufa maji ndani ya ziwa Victoria.

Boti hilo lililokuwa limebeba abiria, mizigo ya shehena ya matenga ya nyanya limepinduka na kuzama ndani ya ziwa Victoria majira ya saa 9:00 usiku baada ya kupigwa na dhoruba iliyoambatana na upepo mkali. 

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Christopher Fuime kwa vyombo vya habari imesema kuwa watu watatu walifanikiwa kuokolewa na wavuvi wa dagaa ile hali watu wengine watano hawajulikani walipo.

Juhudi zaidi za kuwatafuta zingali zikiendelea na Kaimu Kamanda Fuime amewataka wananchi walio kando kando ya ziwa Victoria kutoataarifa iwapo wataona miili ya watu hao ikiwa imeibuka juu ya maji.

TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUWAPATIA KADRI ZITAKAVYO  TUFIKIA.
By Albert G. Sengo
Mwanza.

No comments :

Post a Comment