Airtel yagawa vitabu kwa shule ya sekondari ya Bwelanyake Karagwe
Airtel Tanzania
imeendelea na mradi wake wa kusambaza vitabu katika shule ya Sekondari
nchini chini ya mradi wa ‘Shule yetu’ ambapo shule mbalimbali za
sekondari nchini zimenufaika na mradi.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari, Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania,
Hawa Bayumi alisema kampuni ya Airtel inaendelea kukabiliana na
changamoto katika sekta ya elimu nchini hasa tatizo la vitabu vya kiada
kwa shule za sekondari.
Kupitia
mradi wa ‘Shule yetu’ watoto wengi wa kike watanufaika kwani mradi huu
unalenga hasa katika kumkwamua mtoto wa kike kutoka katika ujinga,
umaskini na maradhi,”
Hawa
aliongeza kwa kusema Leo tunatoa msaada wa vitabu kwa shule ya
sekondari ya Bwelanyake hapa Karagwe Bukoba ikiwa ni mwendelezo wa
shughuli zetu za kijamii katika kupambana na tatizo la vitabu mashuleni.
Vitabu hivi vitawawezesha wanafunzi wa shule ya Bwelanyake kupata
nafasi ya kujifunza na kujisomea na kuwawezesha walimu kupata nyenzo
muhimu za kufundishia.
Kwa
upande wake Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe bi
Siberia Ruboha alisema “elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo tunawashukuru
sana Airtel kwa kushirikiana na Serikali kupunguza tatizo la vitabu vya
kiada vya shule za sekondari hapa nchini. Tunaamini msaada huu wa
vitabu tulioupata leo utasaidia katika kuinua kiwango cha ufaulu na
kuongeza taaluma zaidi kwa wanafunzi wetu na kuongeza idadi ya wanafunzi
wa masomo ya sayansi hapa shuleni. /Nachukua fursa hii kuwaomba
wanafunzi wavitumie fursa hii kujisomea na wavitunze vitabu hivi ili
viweze kutumika na wanafunzi wengi zaidi na kutoa matunda bora na mengi
zaidi.
Mpaka
sasa Airtel kupitia mradi huo imewafikia shule takribani 900 za
sekondari nchi nzima kwa kuzipatia vitabu vya kiada hasa kwenye masomo
ya Fizikia, Hisabati, kemia na Biolojia. mradi huu wa Shule yetu
unasambaza vitabu kwa shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka
cha nne pamoja na vitabu vya walimu kwa ajili ya kufundishia.
No comments :
Post a Comment