Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, August 14, 2013

KAGASHEKI CUP 2013: KASHAI FC 1 vs RWAMISHENYE FC 2, TIMU YA KASHAI YAPEWA KIBANO, YACHINCHWA 2-1 NA RWAMISHENYE!! SASA FAINALI NI BILELE FC NA RWAMISHENYE FC JUMAMOSI HII!!!



Timu zikiingia uwanjaniWachezaji wakisalimiana muda mchache kabla ya mtanage kuanza
Wachezaji wakisalimiana muda mchache kabla ya mtanage kuanza
Wachezaji wa timu ya Kashai wakiomba uwanjani
Wachezaji wa Rwamishenye.

Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya Rwamishenye imeibuka Shujaa na kufanikiwa kutinga
katika hatua ya fainali ya michuano ya KAGASHEKI CUP 2013 baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Kashai Fc. Rwamishenye ndio walioanza kufunga bao kupitia mshambuliaji Khalid Seleman  kipindi cha kwanza nao Kashai wakiongeza bidii na kuweza kusawazisha bao hilo kipindi hicho hicho cha kwanza  kupitia mchezaji wao Paulo Manu. Kipindi cha kwanza kikimalizika timu zote zikiwa nguvu sawa.

Kipindi cha pili kilitawaliwa na timu ya Rwamishenye huku wachezaji wa timu ya Kashai Fc wakizembea kukaba wenzao na kuchoka wachezaji wa Rwamishenye wametumia nafasi hiyo na kuweza kuwaongezea bao la pili kupitia mchezaji wao matata Hassan Hussein aliyeingia kipindi cha pili kwa mkwaju mkali uliompita mlinda mlango wa timu ya Kashai katika dakika ya 75.

Ushindi huu walioupata Rwamishenye unawawezesha kutinga hatua ya Fainali siku ya Jumamosi hii tarehe 17 Agosti kuwavaa washindi walioifunga timu ya Makhirikhiri (Kitendaguro Fc) jana ambao ni Bilele FC katika uwanja wa Kaitaba.

Mchezo huu pia umeweza kuingiliwa na sintofahamu baada ya mashabiki wa timu ya Kashai Fc kuanza kufanya vurugu na kurusha mawe dakika za mwishoni baada ya kuona timu yao imefungwa na jambo hilo limeweza kunyamazishwa na askari waliokuwa uwanjani humo na kuweza kuwaokoa wachezaji na waamuzi wa mtanange huo wasidhurike.
Waamuzi wa mtanange huu
Kikosi cha timu ya Rwamishenye kilichoanza
Mtanange ukiendelea...punde!!
Hatari kwenye lango la timu ya Rwamishenye..

No comments :

Post a Comment