Mmoja kati ya
wanawake wakazi wa Mlowa akichangia katika mkutano huo kwa kutaka
wanaopandikiza chuki za kidini kupewa adhabu kali.
WAFUGAJI jamii ya kimasai na Mang'ati
wakazi wa Mlowa jimbo la Isimani wilaya ya Iringa vijijini mkoani
Iringa wametaka katiba mpya ijayo kuwaweza kuwatetea wafugaji kwa
kuingiza kipengere kitakachowaruhusu wao kuingia katika hifadhi ya
Taifa ya Ruaha kuwasaka simba wanaoua mifugo yao kuwaua.
Wafugaji hao walitoa maoni hayo juzi
katika ofisi za serikali ya kata wakati wakichangia rasmu ya
katiba mpya zoezi lililoendeshwa na kituo cha msaada cha sheria na
haki za binadamu.
Walisema kuwa Simba wameendelea
kuwatesa na kila wakati wanaendelea kuua mifugo yao na pindi
wanapofanya msako wa kuwasaka askari wa wanyamapori wanawachukulia
hatua kali .
Hivyo walisema ili katiba ijayo
iweze kutambua haki za wanyama wengine na pia kutambua uwepo wa
wafugaji ni vema kuingizwa kipengere kinachowapa nafasi ya kuwaua
simba wanaokula wanyama wao.
Mbali ya kutaka kuwekwa kwa
kipengere hicho bado wafugaji hao walitaka kutambuliwa rasmi na
katiba ijayo badala ya ilivyo sasa ambapo wamekuwa wakihamishwa
kama wanyama .
Pamoja na wafugaji hao kwa upande wake
wananchi wa kawaida wameeleza kusikitishwa na hatua iliyofikiwa ya
mchakato huo wa katiba mpya hatua ya kukusanya maoni juu ya rasmu
wakati wao hata katiba iliyopita hawaijui na rasmu hiyo hawajapata
kuoina. |
No comments :
Post a Comment