Mashabiki wa timu ya Simba wakifuatilia moja ya mechi za timu yao katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
TIMU ya soka ya Rhino Rangers imechimba mkwara mzito
juu ya mashabiki watakaojitokeza kwa ajili ya kuangalia tamasha kubwa la muziki
la FIESTA katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi usiku wa leo.
Mkwara huo umetokana na kutokuwa na imani na watu
ambao watakuwa katika uwanja huo utakaotumika katika mchezo wa kwanza wa timu
hiyo dhidi ya Simba SC.
Uongozi wa Rhino, ambayo inamilikiwa na Jeshi,
hautaki kuona uwanjani hapo (pitch), ili uwanja huo uweze kuwa salama kwa ajili
ya mchezo wao wa kesho, ambapo wanaiogopa Simba wakidai inaweza kuweka vitu
vyenye imani ya kishirikina.
Nyumba ya Michezo na Burudani lilidokezwa kuwa hali
hiyo imetokana na maafande hao kuwaogopa Simba katika Nyanja ya ufundi nje ya
uwanja, ambapo wamejipanga kuanza kwa ushindi wa nyumbani.
"Hali kwa sasa iko hivyo hapa, na mashabiki
wote ambao watajitokeza katika tamasha la Fiesta wameshawekewa maonyo uwanja
mzima kuwa hawatatakiwa kugusa eneo la kuchezea mpira, na maafande wenyewe
wameimarisha ulinzi," alisema mwandishi wetu wa Tabora.
Wakati hali ikiwa hivyo mkoani Tabora, Uwanja wa
Taifa hali ni shwari, ambapo mabingwa watetezi, Yanga watakuwa na kazi ngumu
mbele ya vijana waliopanda kwa mara nyingine katika ngazi ya Ligi Kuu, Ashanti
United.
Endelea kutembelea katika mtandao wako wa Nyumba ya Michezo na Burudani kwa mambo mengi zaidi kuhusu Ligi Ku na Burudani kwa ujumla.
No comments :
Post a Comment