Baadhi
ya watumishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakiwa katika
picha ya pamoja katika banda lao lililopo ndani ya Viwanja vya Nzuguni
Mjini Dodoma yanapofanyika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima Nane Nane.
Mwaka huu TCRA wanakuambia 'FUTA-DELETE' ujumbe wowote usio na maana
katika simu yako au mtandao wa Barua pepe. Ila Father Kidevu Blog,
inaongezea Ujumbe 'PUUZIA-IGNORE' taarifa yeyote isiyo na manufaa kwa
jamii katika Mitandao ya Kijamii.
Naibu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mwasiliano Tanzania (TCRA) anaeshughulika na
Uratibu wa Kanda, Victor Nkya akitoa elimu ya FUTA-DELETE kwa vijana
waliotembelea banda hilo leo.
Kikosi
kazi cha Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania Standard Newspapers
(TSN) Limited ambacho kipo ndani ya viwanja vya Nzuguni katika Banda la
Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo katika Maonesho ya siku ya
Wakulima Nane Nane yaliyoanza Agosti Mosi na kutaraji kumalizika Agosti
8, 2013 kitaifa Mkoani Dodoma. Kushoto ni Afisa Masoko, Francis Kihinga
akiwa na Afisa Mauzo na Masoko, Chikira Mgheni. TSN ndio wachapishaji na
wasambazaji wa Magazeti ya Daily News, Sunday News, HABARILEO,
HABARILEO Jumapili na SpotiLEO.
Afisa
Masoko wa TSN, Francis Kahinga akigawa majarida ya Elimika na Academy
kwa wanafunzi walio tembelea banda la TSN. TSN ndio wachapishaji na
wasambazaji wa Magazeti ya Daily News, Sunday News, HABARILEO, HABARILEO
Jumapili na SpotiLEO.
Kampuni
Kongwe ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) nayo ipo katika Viwanja
vya Nzuguni, kuelimisha umma juu ya huduma zake. Pichani ni Maofisa wa
Kampuni hiyo Thomas Lemunge ambaye ni Afisa Biashara wa Mkongo wa Taifa
wa Mawasiliano (katikati) akitoa elkimu kwa mwananchi huku Afisa Habari,
Amanda Luhanga akifuatilia.
Wafanyakazi mbalimbali wa TTCL wakiwa bandani hapo wakitoa elimu ya huduma zao.
Ofisa Masoko na Utafiti wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
Arusha (AICC), Linda Nyanda, akiwapa maelezio wanafunzi wa kidato cha tatu
wa Sekondari ya Maria de-Mathias ya mjini Dodoma juu ya shughuli mbalimbali za
AICC walipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wakulima nane nane katika
Uwanja wa Nzuguni mjini Dodoma.
Ofisa Habari Mwandamizi na Itifaki wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
Arusha (AICC), Catherine Kilinda akiwapa maelezio wanafunzi wa kidato cha tatu
wa Sekondari ya Maria de-Mathias ya mjini Dodoma juu ya shughuli mbalimbali za
AICC walipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wakulima nane nane katika
Uwanja wa Nzuguni mjini Dodoma.
Afisa
Mauzo wa Kampuni ya YARA Tanzania Limited, Catherine Assenga (kushoto)
akimsadia mwananchi aliyetembelea banda lao lililopo ndani ya Banda la
NMB katika Viwanja vya Maonesho Nane Nane, Nzuguni Mjini Dodoma. YARA
ndio wasambazaji wa Mbolea CHAPA MELI.
No comments :
Post a Comment