Afisa
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd Rhys Torrington akitia saini mkata wa
kuonyesha Ligi Kuu ya Tanzania Bara moja kwa moja kupitia Azam TV.
Katikati ni Makamu rais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF Bw. Athuman
Nyamiani.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd Rhys Torrington (kulia) na Makamu wa
rais wa TFF Athuman Nyamiani baada ya kutiliana saini mkataba huo.
Kampuni
ya Azam Media sambamba na Shirikisho la Soka Tanzania TFF zimetiliana
saini mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara moja kwa
moja katika msimu huu wa 2013/2014.
Kampuni
hiyo ya Azam imesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuonyesha mechi hizo
kupitia Azam TV wenye thamani ya shilingi 5,560,800,000/= ambao utalipwa
kwa awamu tatu.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam wakati wa kutia saini makubaliano hayo, Makamu
Rais wa TFF Bw. Athuman Nyamiani amesema Shirikisho la Soka limefurahi
kushirikiana na Azam Media na kuwa hatua hiyo ya kuonyeshwa kwa mechi
hizo itazisaidia klabu kujitangaza na kupata wadhamini wa ndani na nje
ambako Azam TV itakuwa ikionekana.
Naye
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd Rhys Torrington amesema
king’amuzi cha Azam TV kitaanza kupatikana hivi karibuni kwa bei nafuu
na kitakuwa na chaneli zaidi ya 50 huku ligi kuu ikiwa moja wapo.
Ameongeza
kuwa ni lengo la kampuni ya Azam Media Ltd kulifanya soka la Tanzania
kujulikana na kuwa maarufu barani Afrika na kimataifa kwa ujumla.
No comments :
Post a Comment