George Foreman akicheza na michael moore |
George Foreman mbali na ngumi pia mtaalamu wa mapishi
George Foreman
Mtu aliyepata umaarufu, umilionea kwa ngumi
Jina: George Foreman
Alizaliwa: Januari 10,1949 Mahali: Marekani
Ameoa
Kazi: Bondia aliyestaafu, ametwaa ubingwa wa dunia mara mbili wa uzito wa juu, Bingwa wa zamani wa Olimpiki, ordained Baptist minister, ni mwandishi na mfanyabiashara.
UNAPOTAJA majina ya mabondia waliowahi kutamba katika ulimwengu wa masumbwi huwezi kuliacha jina la George Foreman.
Hu ni miongoni mwa mabondia waliotesa katika ngumi za kulipwa za uzito wa juu duniani.
Wababe wengine walinakumbukwa kutokana na uwezo wao wa kutwangana ni Muhammad Ali, Joe Frazier na Mike Tyson.
Hawa ni wachezaji ngumi ambao walikuwa na uwezo usiokuwa wa kawaida katika enzi zao na wana historia ya kuwaelezea.
George Foreman au George Edward Foreman amepata mafanikio mengi ulingoni na kuweza kutengeneza jina lake na fedha kutokana na ngumi.
Ni miongoni mwa mabondia wanaotajwa kuwa matajiri, utajiri wake unakadiriwa kufikia pauni milioni 253.
Amewahi kutwaa ubingwa wa dunia wa udioto wa juu duniani mara mbili, kabl ya hapo aliwahi kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki 1968 .
Ukiongeza na hilo anatajwa kuwa ni bondia aliyeweka historia ya kupigana hadi kuwa na umri mkubwa zaidi wa miaka 48 ambapo alistaafu.
Katika upiganaji wake, alistaafu akiwa na rekodi kucheza mapambano 76 kati ya hayo akiwa amepoteza matano 5 na kushinda mengine yaliyosalia, 68 ikiwa kwa knockouts.
Ni miongoni mwa mabondia waliojiwekea hesima katika mchezo huo na kutambuliwa na Jumba la wanasumbi Bora Duniani na Pamoja na Jumba la Kimataifa la mabondia maarufu.
Foreman ametajwa na Oganaizesheni ya Kimataifa ya utafiti wa Ngumi (IRBO) kama ni bondia wa uzito wa juu wa nane ambaye ni mzuri kwa wakati wote.
Kwa upande mwingine, Foreman alitajwa kuwa mmoja kati ya wapiganaji 25 wazuri katika wa miaka 80 iliyopita akiwa katika nafasi ya tisa kwa ubora katika orodha ya Jarida la The Ring la 2002.
Baada ya kustaafu ngumi, Foreman alijiigiza katika kupromoti George Foreman Grill. Hii imekuwa ikitumiwa na watumiaji karibia milioni 100 sehemu mbalimbali duniani.
Mpiganaji huyo Foreman aliuza haki ya kutumi jina lake na kujiingiza kiasi cha dola milioni 138 .
Foreman aliionesha dunia kuwa anaweza kuwa anavyotaka katika kitu chochote anachofikiria licha kukua katika mazingira magumu wakati wa utoto wake.
Anabainisha kwua alilazimika kuchishwa shule alipokuwa na umri wa miaka 15 na akaanza kufanya kazi. Kisha alihamia Pleasanton, California kwa kusaidiwa na mmoja wa wasimamizi na akiwa huko ndipo alianza kucheza ngumi.
Foreman alikuwa na safari ndefu na ngumu katika mchezo huo kabla ya kutambulika na kupata mafanikio, lakini kila kitu alichopitia kimefanya awe na thamani .
"HIki ni kipaji changu. Niliachana na hisia hasi za upande wangu na kuwa kama bata nje ya maji.Kama si kitu kizuri sikuwahi kusikia. Kama unaweza kukabiliana hali hiyo, kupigana kunakuwa rahisi."
"Unaweza kuwana mke mtalaka au mume mtalaka lakini huwezi kuwa na mtoto mtalaka. Ninataka kuendelea kupigana kwa kuwa ni kitu pekee kinachoniondoa na mambo mabaya. Kama sitapigana ninaweza kuila dunia hii."
"Watoto wangu wote nimewaita George Foreman. Wote wanajua wametoka wapi. Siwezi kukumbuka muda ambao sikuwahi kuingia katika mapigano."
Vitu anavyopenda
Ni Huffman anapenda kufuga na kuendesha farasi
Magari
George Foreman anamiliki magari mawili ambayo anayapenda ambayo ni custom-made lincoln continental.
Pia anamiliki gari jingine aina ya Rolls Royce
Kuchangia jamii
Anamiliki mfuko wa Bony Pony Ranch ambayo ni taasisi isiyokuwa ya kibiashara iliyoasisiwa na Dk. Frank Ryan. unasaidia vijana wanaoishi katika mazingira magumu na kusaidia watoto wenye vipaji ili kutimiza malengo yao.
Red Cross (Msalaba Mwekundu)
Kwa sababu kuna matatizo mengi sehemu mbalimbali duniani na seikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu, Msalaba mwekunsu ni moja ya taasisi ambayo kila wakati imekuwa ikijitokeza na kusaidia watu.
Taasisi hiyo imekuwa ikifanya maandalizi kwa kukusanya misaada kwa ajili ya kusaidia pale yanapotokea matatizo ya dharura. Inahakikisha inalinda maisha na uhai wa wahanga wa vita na vurugu za ndani. Bonsi huyu wa zamani ni mmoja wanaochangia misaada katika taasisi hii muhimu.
Anapenda kufuga mbwa
George Foreman anapenda kufunga mbwa, anasema na ambwa 11 wenye asili ya Ujerumani aina ya shepherd.
Anasema. Sijawahi kukaa bila ya kuwa na mbwa wangu wamekuwa wakikaa katika kila kona ya nyumba na mke wangu hawezi kuruhusu kuwa na zaidi ya mbwa hao.
Lakini nina mbwa wengi. Ninawafuga. Kila wakati ninakuwa na mbwa wadogo. Ninapenda mbwa wa wa Kijerumani aina ya shepherd."
George Foreman anapenda kuvaa saa aina ya Hublot.
Makala haya yametayarishwa na mwandishi Deodatus Myonga wa gazeti la JAMBO LEO kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya mtandao
No comments :
Post a Comment