Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, August 23, 2013

HATIMAYE MWANAMUZIKI MKONGWE WA DANS MUHIDIN GURUMO AKUBALI YAISHE NA SASA ASTAAFU RASMI MUZIKI



Mwnamuziki mkongwe wa muziki wa dansi wa bendi ya Msondo Ngoma, Mzee Muhidin Gurumo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake wa kustaafu rasmi kazi ya muziki aliyoifanya kwa muda wa miaka 53 sasa. Gurumo alitoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Picha na Magreth Kinabo.
************************************
Na Jennifer Chamila, Maelezo.
MWANAMUZIKI mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo amestaafu rasimi kazi ya muzika alioifanya kwa muda wa miaka 53.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mzee  Gurumo mwenye umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa.
“Muziki kwangu umekuwa kama asili yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu kutokana na umri wangu na nitabaki kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki yeyote atakayetaka ushauri wangu,”alisema  Mzee Gurumo.
Pamoja na kufanya kazi ya muziki Gurumo alisema kuwa hakupata mafanikio makubwa zaidi ya kujenga nyumba anayoishi na familia yake.
 “Mimi  nimeimba kwa muda mrefu sana lakini hata baiskeli sina,”alisema Mzee Ngurumo. Hata hivyo alisema  nashukuru kuwa ana nyumba ya kuishi na familia.
Vilevile Mzee Gurumo amewaasa vijana kuwa wabunifu na kuupenda mziki wa zamani kwani ndio chimbuko la bongofleva na kuwashauri wanamuziki wa sasa kuwa wavumilivu kukaa muda mrefu kwenye bendi moja ili hata wanapoondoka mchango wao uthaminiwe.
 Mzee   Gurumo  ambaye ana mke na watoto wanne alisema kuwa katika maisha yake ya muziki alifanikiwa kutunga nyimbo 60,000 na anavutiwa zaidi na mwanamziki Hussein Jumbe na Hassani Lehan Bichuka na kwa wanamuziki wa kizazi kipya anavutiwa na Nassibu Abdul ’Diamond’. 
Mwanamuziki huyo mkongwe alianza kufahamika katika tasnia ya muziki wa dansi kwenye miaka ya 1960 ambapo mwaka 1964 alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa bendi ya Nuta Jazz na Mlimani Park.
Alidumu na Mlimani Park mpaka mwaka 1985 na kuhamia Safari Sound aliyofanya nayo kazi mpaka mwaka 1990 na kujiunga na Msondo Ngoma mpaka sasa alipoamua kutangaza rasmi kustaafu kazi hiyo ya Kimuziki.

No comments :

Post a Comment