Bingwa wa Olimpiki katika mbio za masafa marefu za Marathon Mkenya Samuel Wanjiru ameaga dunia.
Duru za polisi zinasema, Wanjiru alikumbana na mauti baada ya kuruka kutoka kwenye chumba chake cha ghorofa moja eneo la Nyahururu, mkoa wa Kati wa Kenya.
Idara ya polisi imethibitisha kifo hicho na kusema uchunguzi umeanzishwa ili kubainisha sababu za kifo hicho.
Mwanariadha huyo alishinda medali ya dhahabu katika mbio za Olimpiki mwaka 2008 mjini Beijing, kwa kuweka muda wa 2:06:32. na kuandikisha rekodi ya kuwa Mkenya wa kwanza kushinda mbio za marathon kwa upande wa wanaume .
Wanjiru pia alikuwa bingwa wa ulimwengu katika misururu ya mbio za marathon maarufu kama world marathon ,ajors kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2010.
Wanjiru pia aliweka rekodi ya mbio za kilomita 21 kwa kuandikisha muda wa dakika 58:33.
Mwezi DeSemba mwaka uliopita Wanjiru alifikishwa mahakamaNI, kwa mashtaka ya kutishia kumwuua mkewe, kumjeruhi mlinzi wake wa nyumbani na pia kumiliki bunduki aina ya AK-47 bila idhini ya serikali.
Mapema mwaka huu Wanjiru alipata ajali mbaya katika barabara inayotoka Nairobi kuelekea Nyahururu, hatua iliyomfanya kujiondoa kutoka kwenye mbio za London Marathon.
No comments :
Post a Comment