Hispania imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza katika viwango vya soka vya FIFA katika viwango vilivyotolewa mapema leo huku nafasi ya kwanza hadi ya kumi ikiwa haina mabadiliko, wakati Afghanistan ikitajwa kuwa ndiyo taifa pekee ndiyo lililopanda kwa nafasi nyingi zaidi.
Afghanistan ambayo ilishinda 1-0 dhidi ya Sri Lanka katika mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa uliyochezwa mwezi uliyopita imeweza kupanda hadi kufikia nafasi ya 164.
Afghanistan mwaka huu imefanikiwa kushinda michezo mitatu na kushinda yote, michezo mingine miwiili ilikuwa ni dhidi ya Bhutan – na kuweza kupanda ngazi tangu walipoanza rasmi kucheza soka la kimataifa mnamo mwaka 1948.
Kwa upande wa vinara, Uholanzi inashika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa wa Dunia na Ulaya, Hispania huku Brazil ikishika nafasi ya tatu, Ujerumani nafasi ya nne na Argentina nafasi ya tano.
England imebaki nafasi ya sita baada ya kuwa na matokeo mabaya katika fainali za kombe la Dunia zilizofanyika nchini Afrika Kusini mwaka jana.
Ghana inashika nafasi ya 15 ikiwa ndiyo taifa toka Afrika ikishika nafasi ya juu huku Japan ambayo inashika nafasi ya 14 ndiyo taifa linaloshika nafasi ya juu toka Bara la Asia.
Mataifa sita yanashika nafasi ya 202 na ndiyo mataifa ya mwisho katika ulimwengu wa soka ambayo ni Andorra, San Marino, Anguilla, Montserrat, American Samoa na Papua New Guinea.
Katika mabano ni nafasi zao zilivyokuwa mwezi uliyopita.
1. (1) Spain
2. (2) Netherlands
3. (3) Brazil
4. (4) Germany
5. (5) Argentina
6. (6) England
7. (7) Uruguay
8. (8) Portugal
9. (9) Italy
10.(10) Croatia
No comments :
Post a Comment