MKONGWE wa soka Duniania mzaliwa wa Brazili Pele kwa mara nyingine tena amehoji dhidi yam kali wa soka wa Barcelona Lionel Messi na kusema kwamba hajawa na mafanikio makubwa ya kuweza kumlinganisha na wakongwe wengine waliyowahi kutamba katika soka ulimwenguni.
Messi, mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or kwa misimu miwili iliyopita amekuwa akifahamika zaidi kuwa ndiye mwanasoka bora kwa sasa duniani. Lakini pia pia kuna madai kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 anataka kuwa mwanasoka bora wa muda wote kama alivyo Pele.
Hata hivyo, Pele amekataa kuamini hivyo na kumataja Messi kuwa ni mchezaji wa kiwango cha chini katika timu ya taifa ya Argentina.
Kwa mujibu wa gazeti maarufu nchini Chile La Tercera, mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Santos amesema hafanan na hao watu ambao Messi amewataja kuwa anataka kuwa na mafanikio ya juu katika soka huku akiwasahau watu waliyofanya makubwa kama kina Johan Cruyff, Michel Platini na Alfredo Di Stefano, ambao walikuwa bora zaidi ya Lionel Messi.”
No comments :
Post a Comment