Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, May 18, 2011

SIMBA v WYDAD KUCHEZA CAIRO


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 18, 2011

SIMBA v WYDAD KUCHEZA CAIRO
Mechi ya kutafuta timu itakayocheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika
kati ya Simba ya Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco itachezwa Mei 28 mwaka
huu kwenye Uwanja wa Petrosport jijini Cairo, Misri. Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) liliamua mechi hiyo ya mkondo mmoja ichezwe uwanja huru
(neutral ground).

Iwapo muda wa kawaida wa dakika 90 utamalizika kwa sare, mshindi atapatikana kwa
mikwaju ya penalti. Wenyeji wa mechi (kwa maana ya kupokea timu na viongozi
uwanja wa ndege) ni Chama cha Mpira wa Miguu cha Misri (EFA).

Gharama nyingine zozote zitabebwa na timu husika kupitia vyama vyao-Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocco (FRMF).


Kila timu itajigharamia usafiri wa kwenda Cairo, pamoja na gharama za malazi.
EFA imeombwa kusaidia timu zote katika maandalizi ya hoteli za kufikia.

Gharama za maofisa wa mchezo (waamuzi na kamishna) ikiwemo usafiri na malazi
zitabebwa na klabu hizo kupitia vyama vyao (TFF na FRMF). Gharama zozote ambazo
EFA itatumia katika maandalizi ya mechi hiyo zitarejeshwa na TFF na FRMF.

Pia mapato yatakayopatikana kutokana na viingilio katika mechi hiyo, EFA
itayagawa nusu kwa nusu kwa klabu hizo kupitia vyama vyao vya mpira wa miguu-
TFF na EFA.



Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

No comments :

Post a Comment