Uongozi wa Klabu ya Yanga umefanikiwa kupata Ngao mbili zenye hadhi ya kimataifa ikiwemo ngao ya Malkia Elizaberth wa Uingereza iliyopatikana Mwaka 1953 na nyingine iliyoshindaniwa katika miaka ya 1954.Taarifa hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Celestine Mwesigwa ambaye Ngao hizo ni hazina ya Klabu ya Yanga katika kuweka kumbukumbu ya Yanga ikiwemo na vitu vingine.“Baada ya kupata Ngao hizi ipo haja ya kuwatafuta wazee waliowahi kuiongoza Klabu yetu ama waliocheza ili tuweze kupata uhakika na Ngao hizi tulizozipata.”Mwesigwa.
Katibu Mkuu ametoa wito kwa wanachama na wadau wote wa Yanga kujitokeza kwa wingi kama kuna mtu ana taarifa yoyote kuhusu Ngao hizo pamoja na zawadi mbalimbali ambazo watu wanazo majumbani kwao kuvirejesha mara moja katika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga.
Hivi karibuni uongozi wa Yanga umeonyesha nia ya kuweka mikakati ya kuanzishwa eneo la kutunzia kumbukumbu mbalimbali za Klabu ya Yanga vikiwemo Vikombe mbalimbali,Ngao pamoja na tuzo za wachezaji na viongozi.
No comments :
Post a Comment