Mratibu wa pambano hilo Kaike Siraju |
Mabondia Mada Maugo (kushoto) na Francis Cheka Kulia, katikati ni Mratibu wa Pambano la wakali hao Kaike Siraju |
MABONDIA Francis Cheka na Mada Maugo wanatarajia kupanda ulingoni ka mapambano mkali siku ya Idd Pili kwa ajili ya kumaliza ubishi wa nani mbabe dhidi ya mwenzake, katika pambano la kuwania ubingwa wa Mabara (UBO) linalotarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa pambano hilo, Kaike Siraju, alisema, tayari mabondia hao wameshasaini mkataba wa kucheza pambano hilo la raundi 10 uzito wa Kati, kilo 72.5
Cheka na Maugo wanacheza pambano hilo ikiwa ni miezi kadhaa baada ya mabondia hao kuzichapa Januari Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa (PTA) na Cheka kuibuka mbabe kwa ushindi wa pointi moja, hali iliyozua malumbano kuwa majaji walimpendelea bondia huyo.
Alisema, pambano hilo litapambwa na mapambano mengine ya utangulizi, ambako Maliki Kinyogoli atazichapa na Deo Njiku raundi 10 uzito wa (Superfly), Seba Temba na Obote Ameme huku Fadhili Majiha akimvaa Sadick Abdul-Aziz raundi sita.
Mapambano mengine yatawakutanisha Doi Miyeyusho na Albert Mbena huku Cosmas Cheka akivurumishana masumbwi na Hoseni Mbonde.
No comments :
Post a Comment