Na Onesmo Ngowi
Masumbwi
au kwa majina mwengine ndondi au ngumi na kwa majina ya mitaani ndogwa,
mawe n.k. ni mchezo unapoendwa sana na watu wengi. Aidha mchezo huu ni
kati ya michezo inayoogopwa sana duniani. Mchezo wa ngumi uko hatarini
kupoteza maana yake ya asili yaani kucheza kama burudani, kuwakilisha
nchi na kujenga ushupavu wa mchezaji. Mamilioni ya watu wanaojazana
kuutazama wasingependa kabisa kujiingiza kuucheza mchezo wa ngumi. Sasa
endelea………………………………….!
MFUMO FEDHA, NA TAA INAYOZIZIMA
Kama
nilivyokwisha elezea hapo mwanzo ngumi zilichezwa kwa ushindani mkubwa
kuwakilisha nchi za mabondia wapinzani. Miaka ya sasa tumeona kabisa
mwelekeo tofauti wa ngumi na ambao kwa kiwango kikubwa kimeushusha
kabisa hadhi mchezo wenyewe.
Mabondia
wengi wa miaka ya sasa toka nchi za Afrika Mashariki wanashiriki tu
kwenye mapambano kwa lengo la kupata fedha za kujikimu.
Wengi
wa mabondia hawa hutoroshwa nchini mwao kimyakimya na mameneja feki
wenye lengo la kuwatumia kujipatia fedha. Mabondia wengi wa zamani
wamegeuka kuwa mawakala feki wa mameneja hawa wenye lengo la kuwatumia
mabondia kwa manufaa yao.
Mabondia
wengi toka nchi za Afrika Mashariki wamewahi kutapeliwa fedha nyingi na
mameneja / mapromota hawa feki baada ya kucheza mapambano katika nchi
za Ulaya, Asia na hata Afrika.
“Fedha”
na sio kitu kingine chochote kinachokuwa msukumo wa wanamasumbwi wengi
wa Kitanzania kucheza ngumi. Kuna mameneja / mapromota wengi wa nje
wanaosema wazi kwamba wanamtaka bondia wa kushindwa na sio wakushindana.
Hii
ni kwa sababu wanataka kuwatengenezea rekodi nzuri mabondia wao. Yapo
maombi toka kwa mameneja hawa matapeli ambapo wanaomba bondia wa
Kitanzania aandaliwe pambano feki hapa nyumbani ili rekodi yake
ikubalike na shirikisho la nchi yake na hatimaye kumsaidia kumpandisha
viwango bondia wake.
Mchezo
wa ngumi umepoteza mwelekeo sio tu hapa Tanzania bali dunia nzima.
Mameneja / mapromota wengi huwatengeneza mabingwa badala ya kuwaacha
mabondia wake wawe mabingwa wa kweli.
Kwa
kawaida bondia bingwa anatakiwa awe amewashinda mabondia karibu wote
walio kwenye uzito / kiwango chake ndipo ajulikane kama bingwa.
Lakini
mabingwa wa sasa wanatengenezwa toka pambano la kwanza kwa
kupambanishwa na mabondia hafifu ili awashinde na kutengeneza rekodi
nzuri. Wapo mabingwa wengi wa dunia waliotengenezwa kwa njia hii badala
ya kuwa mabingwa kwelikweli. Hii yote ni kwa ajili ya fedha.
Bingwa yeyote anapotakiwa atetee ubingwa wake hupewa donge nono. Kwa bingwa
anayetambuliwa na mshirikisho kama WBA, IBF, WBO na WBC donge la fedha
analopewa ni kubwa zaidi. Mameneja wengi hutumia fedha kuwaingiza
mabondia wao kwenye viwango vya mashirikisho haya ili kuwaweka katika
orodha ya kuelekea kwenye ubingwa.
Mara
tu bondia anapokuwa bingwa hujihakikishia ulaji na meneja / promota
wake anamchagulia wapinzani wasioweza kumnyang’anya ubingwa huo ili
aendelee kutulia nao.
Bingwa
huyu anawezza kukaa na ubingwa kwa muda mrefu sana. Mfumo wa sasa wa
ngumi unalenga kuwanufaisha wale walio na bondia kama mamaneja, promota,
wakala, matchmakers na bondia wengine. Mfumo fedha unadidimiza mchezo
wa ngumi.
Kuna
makubaliliano na ushirikiano mkubwa sana wa siri kati ya meneja,
promota na baadhi ya mashirikisho husika ili bondia aweze kuwa bingwa na
atetee ubingwa wake kwa muda mrefu. Hali hii japokuwa inadhibitiwa kwa
kiasi kikubwa miaka ya karibuni bado imechangia kwa kiasi kikubwa
kushuka kwa mchezo huu kidunia.
Miaka
ya karibuni makundi (rackets) kama hizi ziligundulika na kuwekwa wazi
kwenye Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF). Rais wa zamani wa IBF Bob
Lee Sr. pamoja na maofisa wengine walitiwa hatiani kwa kosa la
kuwatengenezea mabondia ulaji kama huu.
Walisemekana
kuwa walidai kiasi cha dola kama 300,000 ili bondia apandishwe kiwango
na achezee ubingwa. Bob Lee Sr. na wenzake walikumbwa na kashfa hii na
kuondolewa IBF.
Japokuwa
mashirikisho mengi ya ngumi bado yanaendelea na uozo huu ni juhudi
ndogo sana zinazofanywa kuwabana. Ilikuwa rahisi kwa IBF kubanwa kwa
kuwa sheria za nchi ya Marekani zilitumika. Mengi ya mashirikisho ya
ngumi yapo nje ya sheria za Marekani na sio rahisi kuwadhibiti. Badala
yake juhudi nyingi zinafanywa na mabondia wachache kwa kufungua kesi za
madai mahakamani ili kuweza kupata haki zao.
Mameneja
/ mapromota nao hawako nyuma kwenye kashfa mbalimbali za ngumi
zinazohusu utumiaji wa fedha za mabondia na hata kuwatibulia kuwa
mabingwa. Ziko kesi nyingi kwenye mahakama huko Ulaya na Marekani ambazo
mabondia wanawadai mameneja / mapromota mamilioni ya fedha. Mara nyingi
kesi hizi humalizwa nje ya mahakama kwa makubaliano.
Sheria
kali zinazoendesha mchezo huu zinatakiwa zifuatwe na udhibiti uwe wa
hali ya juu. Sio rahisi kupata mafanikio katika mchezo huu bila sheria
hizi kufuatwa na kila mdau.
“Niletee
bondia asiye mkali ili asimpe shida bondia wangu. Mtengenezee pambano
la kumpandisha rekodi yake. Mtengenezee leseni mpya inayoonyesha rekodi
nzuri”
Haya
ni baadhi tu ya maelekezo yanayotoka kwa mameneja wa nje wanapotafuta
bondia wa Kitanzania kwenda kucheza huko nje. Kuna kundi kubwa la
mameneja hawa wachwara ambao wanashirikiana na mawakala wa kila aina
hapa Afrika.
Wengi
wa mawakala hawa kama nilivyokwisha eleza hapo mwanzo ni mabondia wa
zamani na wafanya biashara wanaotumia nafasi ya kumpeleka bondia nje ili
wakanyooshe mambo yao.
Inapotokea
safari ya nje kwa bondia wafanya biashara hawa hawawezi hata
kuwa-sekondi (kuwahudumia) mabondia kwenye kona zao na badala yake
wanawaachia wageni wa nchi wanayochezea kufanya kazi hiyo. Ni wazi
kwamba bondia anapohudumiwa na mgeni tena anayetaka ashindwe ana nafasi
ndogo sana ya kufanya vizuri. Wengi wa wahudumu hawa hawaelewani hata
lugha na bondia mwenyewe!
Safari
nyingi za mabondia wetu siku hizi wanatakiwa wasafiri wenyewe ili eti
wawakute wahudumu nchi wanayokwenda. Kwa kawaida kila bondia wanatakiwa
asafiri na meneja na kocha wake. Hii ndiyo kawaida ya safari za mabondia
wa ngumi za kulipwa. Lakini hili halitokei siku hizi.
Iaendelea………………………….!
No comments :
Post a Comment