Sadiki momba (kusshoto) akiwa ulingoni hivi karibuni |
Bondia
mwenye manjonjo, mbwembwe na vituko vingi ulingoni Sadiki
Momba"kijotijoti". amesema anamtamani bondoa, Ramadhan Shauri (ambaye ni
bingwa wa IBF Afrika)', sio alen kamote wa tanga ambaye ni bingwa wa
Afrika mashariki anayetegemea kucheza nae tarehe 27 octoba 2012.
Pambano hilo linaloandaliwa na Ally Mwanzoa, na kuratibiwa na bigright promotion katika ukumbi wa Friends corner hotel-manzese.
Sadiki
momba anasema bondia anayemfikiria ni Ramadhan Shauri na ni bingwa wa
kupewa kwa kutengenezewa mazingira ,"shauri haniwezi na yeye mwenyewe
anajua hata mapromota wakitokea wa kutukutanisha mie nakuwa tayari kwa
gharama zozote lakini Mzazi kocha wa shauri hukataa au utaja dau kubwa
la mamilioni ili promota akimbie,Shauri amecheza mapambano 13,kapigwa
matatu,kadroo moja tisa kashinda wakati mie nimecheza mapambano kumi na
nane(18) droo moja,nimepigwa moja na mudy matumla kwa kubebwa na
yaliyobaki 16 yote nimeshinda hivyo mie nina rekodi nzuri ulingoni
kuliko Shauri.
sijapata
tu nafasi ya hizo mechi za ubingwa lakini hao mabingwa wao wanaowapa
mechi za kimataifa mie nimeshawapiga sana mpaka kuokolewa na refa au
kufikishwa mahospitalini wakiwa hali mbaya kwa kipigo.
Njooni
mumuangalie kamote nitakavyomfanya ndio maana simzungumzii sana najua
nitampiga kirahisi sana akakate viuno vyake kwao tanga.
Naomba
promota yoyote ajitokeze kutuandalia mchezo kati yangu na shauri
wasimtengenezee mazingira na vibonde, tunajua kocha Mzazi na mabondia
wake wanaabudu uchawi hivyo nitawaomba chama kitakachosimamia mchezo
kiwaruhusu waganga wao waloge mpaka ulingoni siku ya mchezo- nasema
hivyo ili mzazi asiogope sana akubali kucheza na mimi kwa imani zake za
kichawi.
Mimi
nijiamini kwa mazoezi yangu na kipaji nilichonacho na nina uwezo wa
kulifanyia taifa letu makubwa kama nitawezeshwa kwa kuandaliwa mapambano
ya kimataifa na ya nje ya nchi, kwani hapa Tanzania karibu mabondia
wote wa uzito wangu nimeshawamaliza,bado sijulikani kwa wakubwa kwa
sababu sijapata mechi za kimataifa.
No comments :
Post a Comment