Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, April 4, 2013

ALLI CHOKI NA EXTRA BONGO,MZEE YUSUPH WA JAHAZI,MSONDO KUNOGESHA BONANZA LA WAANDISHI JUMAMOSI 'Media Day'




 Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania, TASWA, Juma Pinto, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo, katika Mgahawa wa City Sports Lounge, alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya wasanii watakaotoa burudani siku ya Bonanza hilo, (kushoto kwake) ni Menjea Mawasiliano wa TBL, ambao ni wadhamini wakuu wa Bonanza hilo, Doris  Malulu, Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki na wanamuziki wa bendi hiyo, wakiongozwa na Super Nyamwela.
 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo, wakiwa bize kunakili kinachozungumziwa.
 Baadhi ya wanenguaji na wanamuziki wa bendi hiyo, waliohudhuria mkutano huo leo.
Wanahabari wakiwa bize kunasa matukio katika mkutano huo leo
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, akifafanua jambo kuhusu maandalizi ya bendi yake katika Bonanza hilo, wakati wa mkutano huo leo.
*********************************
Na Mwandishi Wetu
 BENDI ya muziki wa dansi ya Extra Bongo na kundi la taarabu la Jahazi Modern ndiyo burudani zitakazonogesha tamasha la vyombo vya habari litakalofanyika Dar es Salaam kesho (Jumamosi).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mchana katika Mgahawa wa City Sports Lounge, wakati wa kutambulisha burudani hizo, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinachoandaa bonanza hilo, Juma Pinto, alisema maandalizi kuhusiana na tamasha hilo linalojulikana kama Media Day Bonanza yamekamilika.
Alisema wameichukua Extra Bongo inayoongozwa na Ally Choki na Jahazi Modern inayoongozwa na Mzee Yusuph kutokana na makundi hayo kuwa juu hivi sasa katika muziki kwa maeneo yao.
“Tunaamini watakaokuja kwenye tamasha watakuwa na furaha ya aina yake na tumejiandaa vya kutosha,” alisema Pinto na kueleza kuwa bonanza hilo litafanyika viwanja vya Sigara Chang’ombe, Dar es Salaam na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Pia Pinto alisema bendi ya Msondo Ngoma Music itapiga kwenye viwanja hivyo kuanzia saa moja usiku baada ya bendi za Extra Bongo na Jahazi kumaliza kutumbuiza Media Day na kwamba imetoa ofa kwa wanahabari watakaotaka kubaki kuendelea kupata burudani mpaka usiku wa manane.

“Msondo wana bonanza lao kila Jumamosi, sasa wamekubali kwamba wanahabari watakaotaka kubaki baada ya bonanza kumalizika jioni wabaki wajiunge na Msondo Ngoma,” alisema Pinto.


Bonanza hilo la TASWA linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) likiwa na lengo la kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu alisema wamejipanga vya kutosha na kwamba wadau wafike kwa wingi kuhakikisha mambo yanaenda kama yalivyopangwa.

“TBL ni mdau mkubwa wa wanahabari, tumewaandalia mambo mazuri, naomba msikose,” alisema Malulu na kuongeza kuwa wanaamini wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari wanaotarajiwa kushiriki bonanza hilo watafurahi vya kutosha siku hiyo.

Naye Choki akizungumza kwenye mkutano huo, alisema vijana wake wamejipanga vya kutosha kushambulia na kuwa dhamira yao ni kuona wana habari wanafurahi vya kutosha na kuwa mambo waliyowaandalia kila mtu atafurahi kuiona Extra Bongo.

No comments :

Post a Comment