Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), kiakabidhi mifuko ya saruji kwa viongozi wa Kata ya Kiomoni.
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MBUNGE
wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), awametaka wananchi wa
mkoa wake kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika shughuli za
maendeleo katika maeneo yao.
Kauli
hiyo aliitoa kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza katika ziara
yake hiyo katika kata za halmashauri ya jiji la Tanga na Wilaya ya
Pangani, ambapo alisema ni muhimu kwa kila mwanajamii kutambua wajibu
wake.
“Suala
la amaendeleo halina itikadi na sasa sio wakati wa kampeni za uchaguzi,
ni jukumu letu kwa viongozi wa Mkoa wa Tanga, kuhakikisha tunashiriki
katika miradi ya maendeleo kwa dhati.
“Ni
wazi Mkoa wa Tanga tuna kila sababu ya kuhakikisha tunaimarisha uchumi
wetu hasa baada ya miaka kadhaa viwanda vyake kufa kutokana na
kutokuwepo na usimamizi mzuri. Ikiwa kila mtu atatambua wajibu wake ni
wazi tutafanikiwa kufikia lengo letu,” alisema Mwidau.
Alisema
kutokana na hali hiyo kila mara amekuwa akishiriki katika kuhamasisha
maendeleo katika maeneo yote ya mkoa huo bila kujali uongozi wa kaa upo
chini ya chama cha CUF au CCM.
“Tanga
tuna ardhi nzuri na tuna kila sababu ya kujivunia jambo hili ingawa
kukosekana kwa usimamizi madhubuti kwetu imekuwa ni kilio kikubwa kwa
wananchi wetu tunaowaongoza, wabunge wote wa mkoa huu tuna wajibu wa
kuliangalia hili,” alisema Mbunge Mwidau.
Katika
ziara hiyo akiwa wilayani Pangani Mwidau, alisema kuwa amefurahishwa
kuona wananchi na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwera kuamua
kuchimba kisima kikubwa zaidi ya kilichopo sasa na katika hilo
amefurahishwa kuona mchango wa awali wa mashine aliyoitoa imewezesha
kujengwa kwa kisima kisima kingine kikubwa cha futi 45 na kipenyo cha
nchi sita.
No comments :
Post a Comment