Timu
nne zitakazochuana katika kipindi cha tatu cha Guinness Football
Challenge wiki hii. Kuanzia kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa
nyekundu), Tanzania –bluu, Uganda- kijani na nyeusi ni timu kutoka
Kenya. Meneja
wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi(kulia) na mtangazaji wa kipindi
cha Tamasha la michezo Amry Masare wakijadili na kufanya uchambuzi wa
kipindi cha kwanza na pili cha Guinness Football Challenge jana katika
kipindi cha Tamasha la michezo kinachorushwa na televisheni ya ITV.
………………………………………………………………
Jumatano iliyopita kupitia
televisheni za ITV na Clouds TV mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL
CHALLENGE™ yalituonesha ni kwanini ushirikiano ni muhimu kwa washiriki
kuonyesha ujuzi wao. Francis Ngigi and Kepha Kimani kutoka Kenya
walifanikiwa kuingia hatua ya mwisho na kujipatia fedha za kimarekani
dola 3,000 shukrani kwa vipaji vyao na ushirikiano mzuri.
Francis na Kepha wana nafasi ya
kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo
wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita cha fedha za kimarekani hadi
kufikia dola 250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano haya
kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne
mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka
mshindi na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki,watatakiwa
kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni
kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya
Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za
ITV na clouds TV. Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu
na dakika kumi na tano(3:15) usiku ambapo Clouds TV itarusha kipindi
hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .
Katika Episodi ya tatu ya
mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na
Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi
itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa?
Majibu yote yatapatikana siku ya Jumatano.
Hizi ndizo timu zitakazochuana
vikali katika kipindi cha pili wiki hii cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE
kinachorushwa na televisheni za ITV na Clouds TV.
Timu ya bluu-Tanzania:
- Mohamed Kobembe na Gullam Sosha wenye umri wa miaka 23 kutoka Dar es Salaam watashirikiana kuona kama wataweza kushinda katika kipindi cha tatu cha GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.Mohamed ndiye kichwa cha timu ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya maswala ya kodi na Gullam ambaye ni mchezaji wa Ndanda FC, wana matarajio ya kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Timu nyekundu-Kenya:
- Kenneth Kamau mwalimu wa timu ya vijana(23) na Willis Ogutu(miaka 30) wote kutoka Nairobi watachezea Kenya.Keneth ataonesha maarifa yake ya soka wakati Willis ataonesha uwezo wake wa kucheza mpira.
Timu ya kijani-Uganda:
- Kennedy Mwota(22) kutoka Naijanakumbi na Steven Nsubuga(25) kutoka Kampala.Kennedy ni mwanafunzi na Steven ni muhasibu.Kennedy ataonesha ujuzi wa soka na steven kipaji chake cha kusakata kabumbu.
Timu nyeusi-Kenya:
- Wafanya biashara wa Nakuru,Stephen Kaguda,35 na Gideon Onyango,34, watavaa jezi meusi. Stephen ambaye ni mshabiki wa Barcelona FC atakuwa akijibu maswali wakati Gideon ambaye ni mshabiki wa Man Utd atachezea mpira.
Wapenzi wa kipindi hiki cha
Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza
kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa
kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.
Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya,
Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufatilia ukurasa huu
‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni
kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya
Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga
yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano
usiku.
Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane. Tafadhali Kunywa kistarabu.
No comments :
Post a Comment