Mwili
wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na
askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva
huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa
ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram
asubuhi ya leo
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi
la uokoaji na wengine wakisubiri kutambua ndugu zao, jambo ambalo
halikupata nafasi.
Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi
---
Inakadiliwa watu zaidi ya watu 18
wamepoteza maisha kufuatia kufukiwa na gema la mchanga/moram wakati
wakichimba na kupakia kwenye malori eneo la Moshono jijini Arusha.
Shuhuda mmoja wa ajali ambae pia
ni mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa kawaida gari ndogo kama
Fuso hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na watu 12 bila kuhesabu
dereva na utingo.
Miongoni wa waliofikwa na mauti ni
pamoja na madereva wa magari hayo. Katika eneo la ajali hali ni ya
simanzi na vilio toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na marafiki na
ndugu wa jamaa waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio.
Meya wa Manispaa Mh Gaudence
Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ni miongoni mwa
viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana na kikosi cha Jeshi
la Wananchi wa Tanzania kufanya uokozi.
Wachina wakipeleka moja ya mashine
zao (Excavator) kuongeza nguvu katika kusaidia kufukua miili ya watu
hao iliyonaswa na kifusi hicho. Picha/habari Kwa Hisani ya ARUSHA255 BLOG
No comments :
Post a Comment