Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, April 5, 2013

‘LOVE AND POWER’ YA KANUMBA KUZINDULIWA JUMAPILI LEADERS






Na Elizabeth John

FILAMU ya aliyekuwa nguli wa filamu nchini, Marehemu Steven Kanumba, inayojulikana kwa jina la ‘Love and Power’ inatarajiwa kuzinduliwa rasmi keshokutwa katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Marehemu Steven Kanumba
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mdogo wa marehemu  Kanumba ambaye pia ni kiongozi wa ofisi yake ya ‘Kanumba The Great’ iliyopo Sinza, Seth Bosco alisema wameamua kuizundua siku hiyo kutokana na kuwa na kumbukumbu ya kutimiza mwaka moja tangu kilipotokea kifo chake.

Alisema zaidi ya waigizaji 10 kutoka Ghana wanatarajia kuwepo siku hiyo ikiwa ni pamoja na rafiki wa marehemu, ambaye ni muigizaji maarufu barani Afrika, Mnigeria, Ramsey Noah.

“Ramsey amethibitisha kuwepo katika uzinduzi huu na anatarajia kuingia nchini kesho (leo),” alisema Bosco.

Akizungumzia ratiba ya siku hiyo ya uzinduzi alisema, itaanzia
nyumbani kwa marehemu, baada ya hapo wataelekea makaburini na baadae Leaders kwa ajili ya uzinduzi huo.

Alisema wapenzi na mashabiki wa filamu za Kanumba wanatakiwa kufika asubuhi nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya ibada ya kumsalia itakayoanza saa nne asubuhi na kuisha saa tano.
Alisema mara baada ya ibada hiyo ndugu, jamaa, marafiki, waigizaji pamoja na mashabiki wake watakula chakula cha pamoja kisha kuelekea makaburini.

Alisema bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta ndio itahusika siku hiyo kwa upande wa burudani, kisha uzinduzi rasmi utafanyika huku kopi za filamu hiyo zikiuzwa hapopapo.

Marehemu Kanumba alifikwa na umauti Aprili 7 mwaka jana nyumbani kwake Sinza Vatcan, huku kifo chake kikihusishwa na msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

No comments :

Post a Comment