Jeffrey Mathebula (kushoto) na Takalani Ndlovu (kulia) katika moja ya mapambano yao.
Mabondia
wa Afrika ya Kusini Jeffrey Mathebula na Takalani Ndlovu watakutana
katika ukumbi wa Carnival City Casino jijini Johannesburg jimbo la
Gauteng nchini Afrika ya Kusini katika pambano la mchujo (Elimination
Title) la ubingwa wa dunia uzito wa unyoya (Featherweight).
Wawili
hawa ni mahasimu wakubwa wanaojulikana nchini Afrika ya Kusini na
walishakutana mara mbili ambapo Ndlovu alishhinda pambano la awali huku
Mathebula akishinda pambano la mwisho.
Wakati
huo huo mabondia Vusi Malinga wa Afrika ya Kusini na Diarh Gabutan wa
Phillipines watakutana katika mpambano mwingine wa mchujo kuwania tiketi
ya kukutana na bingwa wa dunia katika uzito wa Bantam.
Promota
maarufu wa Afrika ya Kusini Branco Milenkovic wa kampuni ya Branco
Boxing Promitions atakuwa ndiye mwandaaji wa mpambano huo utakaofanyika
tarehe 23 mwezi wa tatu mwaka huu.
Huu
ni mwendelezo wa Shirikisho la Ngumi la kKmataifa IBF katika programu
yake ua “Utalii wa Michezo” barani Afrika ambapo imejiwekea lengo la
mapambano 100 ya ubingwa mwaka huu.
No comments :
Post a Comment