Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, April 4, 2013

VODACOM TANZANIA NA FENIX INTERNATIONAL SASA KUWANUFAISHA WATANZANIA WALIOPO NJE YA GRIDI YA TAIFA



  Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa (kushoto) na Meneja wa biashara wa kimataifa wa Fenix International, Peter Glenn wakimshuhudia mkazi wa Kibaha Bi Anna Joseph,wakati akionesha kwa vitendo jinsi chaja mpya aina ya Readyset inavyounganishwa kabla ya matumizi,uzinduzi wa chaja hiyo inayotumia  nishati ya jua,ina uwezo wa kuchaji simu zaidi ya 10 kwa siku, matumizi ya redio, kuzalisha mwanga wa hadi masaa 30. Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya kifaa hicho hususan kwa maeneo yaliyo nje ya gridi ya Taifa umefanyika Dar es Salaam kupitia ubia baina ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Fenix International.
Mkazi wa Pangani, Wilaya ya Kibaha, Pwani, Anna Joseph, akionesha waandishi wa habari jinsi ya kutumia aina mpya ya chaja inayotumia nishati ya jua 'ReadySet' iliyozinduliwa Dar es Salaam kwa ushirikiano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom  na Fenix International. Mkazi huyo amewaeleza waandishi wa habari kuwa amekuwa akijipatia kipato cha hadi sh elfu 80 kwa mwezi kupitia kifaa hicho kwa kuchajisha simu za wateja wake.
Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa (kushoto)na mkazi wa Kibaha Bi Anna Joseph ambaye ni mmoja wa wadau walionufaika na huduma ya chaja za Readyset,wakiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namna  chaja hizo mpya na zinatumia nishati ya jua zinavyofanya kazi .   Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya kifaa hicho hususan kwa maeneo yaliyo nje ya gridi ya Taifa umefanyika Dar es Salaam kupitia ubia baina ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Fenix International.   Wanaoshuhudia nyuma ni Meneja wa biashara wa kimataifa wa Fenix International, Peter Glenn, na Mkurugenzi Mtendaji wa Fenix International,nchini,  Peter Mungoma.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa, akisisitizia umuhimu wa kila mtanzania hususan wajasiriamali waishio maeneo yasiyo na umeme kutumia aina mpya ya chaja inayotumia nishati ya jua maarufu Readyset  ambayo pamoja na mambo mengine ina uwezo wa kuchaji simu zaidi ya 10 kwa siku, matumizi ya redio, kuzalisha mwanga wa hadi masaa 30. Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya kifaa hicho hususan kwa maeneo yaliyo nje ya gridi ya Taifa umefanyika Dar es Salaam kupitia ubia baina ya Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom na Kampuni ya Fenix International
  Mkurugenzi Mtendaji wa Fenix International, Peter Mungoma akionyesha kupitia 'projector' aina mpya ya chaja inayotumia nishati ya jua, maarufu kama 'ReadySet  Charger' ambayo pamoja na mambo mengine ina uwezo wa kuchaji simu zaidi ya 10 kwa siku, matumizi ya redio, kuzalisha mwanga wa hadi masaa 30. Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya kifaa hicho hususan kwa maeneo yaliyo nje ya gridi ya Taifa umefanyika Dar es Salaam kupitia ubia baina ya Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom na Kampuni ya Fenix International
---
Dar es Salaam, Aprili 5, 2013 - 
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom imezindua chaja mpya za simu 'Readysety' zinazotumia nishati ya jua na zenye uwezo wa kuchaji zaidi ya simu 5 tofauti kwa wakati mmoja kwa minajiri ya kuwawezesha watanzania hususan waishio maeneo yasiyo na umeme kupata mawasiliano ya uhakika kupitia simu zao za mikononi.

Readysety hizo pamoja na mambo mengine zinatumika kuzalisha mwanga kwa balbu ya aina yoyote kwa matumizi ya nyumbani na mahala pa biashara, na zaidi zina viunganishi kwa matumizi ya umeme wa kawaida.

Kukamilika na hatimaye uzinduzi wa chaja ya ReadySety ni matokeo ya ushirikiano wa kibiashara baina ya Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom nchini na Fenix International baada ya kujiridhisha juu ya ubora na faida zake kwa watanzania hususan wajasiriamali waishio maeneo yaliyo nje ya gridi ya taifa.

Akizungumza katika uzinduzi huo, kwenye duka la Vodacom, MlimaniCity, Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom nchini, Rene Meza, alisema ReadSety zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza fursa za mawasiliano na uhitaji zaidi wa simu za mikononi kwa watanzania waishio maeneo yote mjini na vijijini

"Watanzania waishio nje ya gridi ya taifa, ambao mara kadhaa hupata adha ya kusafiri umbali mrefu pale wanapohitaji fursa za nishati ya umeme kwenye kuchaji simu zao sasa wamepata jawabu," alisema Meza na kuongeza:

"Zaidi ya watu bilioni 1.3 duniani wanaishi bila huduma ya umeme na kuna watumiaji wa simu za mikononi takribani milioni 600 wanaoishi bila kutumia umeme wa gridi kitu ambacho kinawalazimu kutumia karibu dola za Kimarekani bilioni 10 kila mwaka kwa ajili ya kuchaji simu kwa kutumia jenereta na betri za magari," alisema Meza

Aliongeza kuwa Kampuni ya Vodafone na Vodacom ina watumiaji wa simu zaidi ya milioni 100 duniani kote ambao hawajaunganishwa na gridi ya

No comments :

Post a Comment