Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, April 8, 2013

LULU NA MAMA KANUMBA WAONGOZA MAELFU KUWEKA SHADA KWENYE KUMBUKUMBU YA KANUMBA


 


Mama Kanumba na Lulu wakiwa wamekumbatiana baada ya misa maalum ya kumuombea marehemu Kanumba
Mama Kanumba na Lulu wakiwa wamekumbatiana baada ya misa maalum ya kumuombea marehemu Kanumba
Wapenzi wa filamu za kitanzania walioko jijini dar es salaam, leo hii walipata fursa ya kuungana na wasanii mbalimbali wa filamu nchini katika kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja toka kufariki kwa msanii nguli wa filamu nchini Steven Kanumba ambaye alifariki tarehe kama ya leo mwaka mmoja uliopita.
Tukio hilo lilihudhuriwa na watu kibao ambapo pamoja na mambo mengine, watu mbalimbali walipata fursa ya kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la marehemu, wakiongozwa na mama mzazi wa msanii huyo pamoja na binti Elizabeth Michael “Lulu”, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kushiriki katika kifo cha msanii huyo.
Hapa ni baadhi ya picha za tukio hilo kama ambavyo Lenzi ya Michezo imezipokea toka kwa mdau mkubwa wa filamu nchini Oscar Mpejiwa wa Bongo Film Data Base
IMG-20130407-WA007
IMG-20130407-WA008
IMG-20130407-WA006
IMG-20130407-WA005
IMG-20130407-WA004
IMG-20130407-WA003
IMG-20130407-WA002
NDUGU, Jamaa na marafiki wa aliyekuwa Nguli wa Filamu nchini, 
Stive Kanumba, leo wamejumuika kwa pamoja katika kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu staa huyo wa filamu alipofariki 
dunia.

Ikiwa ni mwaka mmoja tangu kutokea kwa msiba huo, leo pia 

mashabiki wa filamu za kibongo waliohudhuria hafla ya 
kumbukumbu hiyo kwa pamoja kuweka mashada ya maua katika 
kaburi la Kanumba, wamewashuhudia Mama Kanumba na 
Msanii Elizabeth Michael 'Lulu' wakiungana na  kuwa kitu kimoja 
na kuondoa tofauti zao na kuadhimisha kumbukumbu hiyo kwa 
kuwaongoza watu waliohudhuria.

Katika Hafla hiyo walihudhuria pia wasanii kibao wa Filam, ambao 

pia walipata fulsa ya kuweka mashada ya maua.

No comments :

Post a Comment