MTANDAO WA WASANII TANZANIA (SHIWATA)
WASANII chipukizi 300 kutoka vikundi 15 jijini Dar es Salaam
wamejitokeza kushiriki maonesho ya kukuza vipaji yaliyoandaliwa na Mtandao wa
Wasanii Tanzania
(SHIWATA) Jumamosi ya Aprili 27 katika ukumbi wa hoteli ya StarLight ,Mnazi
Mmoja Dar es Salaam.
Vikundi ambavyo vimethibitisha kushiriki pamoja na Kaole
Sanaa Group,Splendid,Uyoga Boga na vingine katika fani ya Bongo
Flava,Taarab,Maigizo,Ngoma,Mazingaombwe,Sanaa za Ufundi,Kung
Fu,Sarakasi,Kusheki,Kwaya,na Ngonjera.
Maonesho kama haya yatafanyika kila mwezi na kiingilio ni
bure na vikundi vingine ni Super Shine Morden Taarab,Zijiu,Edeneza Brass
Band,Asili Africa,Mege Arts,Kintu,Army Kwanza,Wachapakazi,Tanhope,Tanz
Arts,Mshikamano,Big House,Lutenga Boys,Kilimasta,Manuary.
Madhumuni makubwa ya tamasha hilo ni kuibua vipaji vya wasanii chipukizi
ili kazi zao ziweze kupata soko hivyo mapromota, Majd,Maproducer wa filamu
wasikoke kufika katika maonesho hayo ili kuona mastaa chipukizi ambao ambavyo
vipaji vyao bado havijaonekana.
Vijana wa sanaa mbalimbali wanatakiwa kufika katika ofisi za
SHIWATA zilizopo Bungoni Ilala ili kujisajili kwa ajili ya maonesho mengine
yanayofuata .
Tanzania
kuna wasanii wengi wenye vipaji lakini kazi zao hazisikiki wala kuonekana
kwenye vyombo vya habari hivyo hiyo ni fursa kutumia maonesho hayo kama soko la
kazi zao katika jiji la Dar es Salaam.
Wasanii mbalimbali ambao vipaji vyao vitakubalika sokoni
watanufaika kupata ajira ya kuuza kazi zao pamoja na kushiriki katika matamasha
mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Peter Mwenda
Ofisa Habari wa SHIWATA
0715/0752 222677
No comments :
Post a Comment