Na Mwandishi Wetu
Bondia Athumani Yanga wa timu ya Ashanti Boxing ya Ilala |
MASHINDANO ya klabu bingwa ya Mkoa wa Temeke yameanza jana
jijini, Dar es Salaam huku
yakishirikisha timu 20 na yanatarajiwa kufikia tamati Aprili 19 mwaka huu.
yakishirikisha timu 20 na yanatarajiwa kufikia tamati Aprili 19 mwaka huu.
Lengo la mashindano hayo yaliyoanza jana ni kuinua vipaji vya
mabondia chipukizi na kupata vipaji bora watakaokuwa chachu ya maendeleo
ya mchezo nchini.
Kocha wa kimataifa wa mchezo huo nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
alisema vijana wanakaoshiriki mashindano hayo walipima uzito katika
Ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke Dar es Salaam.
Super D ambaye pia ni kocha wa timu ya Mkoa wa Ilala ambao ni
waalikwa katika michuano hiyo alisema vijana wake kutoka klabu ya Amana
na Ashanti watafanya vema katika mashindano hayo.
Mkoa wangu umetoa vijana sita ambao naamini watafanya vizuri katika
mashindano hayo na kutoa upinzania mkubwa ambao utakuwa chachu ya
maendeleo ya mchezo huo nchini.
Super D aliwataja baadhi ya mabondia hawo kuwa ni Hussein Mawimbi na Said
Hamisi kutoka klabu ya Amana na Athumani Yanga pamoja na Said Mabunda
kutoka klabu ya Ashanti.
Pia aliwaomba wadau kujitokeza kusaidia mashindano hayo
yanayofanyika katika ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke ili kuhakikisha
hamasa ya kuendeleza mchezo huo inapatikana yatakayofanikisha mafanikio
ambalo ndilo lengo kubwa. la mashindano hayo
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. na Francis
Cheka dhidi ya Japhet Kaseba mapambano yote mawili mbali na hivyo
atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa mabondia ambao awana
wanaweza kumuona na kujipatia vifaa mbalimbali
No comments :
Post a Comment