Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati akitoa ripoti ya faida ya mapato katika utendaji kazi wa benki hiyo kwa mwaka 2012 jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mjumbe
wa Bodi, Ally Laay na Mchambuzi Masuala ya Fedha, Mohammed Warsame. (Picha na Habari Mseto Blog)
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Chales Kimei (katikati) akiwa na
Mchambuzi wa masuala ya Fedha, Prof. Mohammed Warsame, Mjumbe wa Bodi,
Ally Laay, Joyce Nyanza na Mkurugenzi Rasirimali Watu, Dorah Ngaliga.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Uudumu kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
DAR ES SALAAM, Tanzania
IMEELEZWA kwamba mfumuko wa bei umechangia kwa kiasi kikubwa
kushuka kwa uchumi hali inayosababisha mazingira magumu ya utendaji kazi katika
taasisi za kibenki hapa nchini.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati akitoa ripoti ya faida ya mapato
katika utendaji kazi ya mwaka 2012 ambapo alisema kuwa pamoja na kushuka kwa
uchumi benki yake imepata faida ya shs.bilioni 81 sawa na asilimia 113 ambayo
ni kubwa kuliko miiaka ya nyuma.
Alisema faida hiyo imepanda kwa asilimia kubwa tofauti na
mwaka 2011 ambapo walikuwa na faida ya shs. Bilioni 38 na kuongeza kuwa
faida ya mapato kibenki imepungua kwasababau ya hali ya uchumi na ongezeko la
bei.
Kimei alisema kuwa, hali hiyo pia husababishwa na ushindani
wa kibenki ambao umekuwa mkubwa ambapo hadi sasa kuna benki 50 ingawa kabla ya
hapo kulikuwepo na benki 27 nchi nzima.
Aidha, benki hiyo kwa mara ya kwanza katika historia imefanikiwa kufungua tawi nchini Burundi
mwishoni mwa mwaka jana ambako kuna
makao Makuu ya benki ya CRDB pamoja na
matawi madogo madogo na kwamba ndani ya
mwezi mmoja walifanikiwa kupata faida ya shs.bilioni 1.2 .
No comments :
Post a Comment