Mashindano ya Kombe la Challenge yatakayoshirikisha jumla ya Timu sita kwa timu za Afrika Mashariki na kati yanatarajiwa kufanyika Desemba 14 hadi 27 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za TFF Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kandanda hapa Nchini Tff Fredrick Mwakalebela amesema jitihada zote zimekamilika kwa kuweza kuziandikia Timu barua ya mualiko kuziomba kushiriki Mashindano hayo na endapo yakienda sawa watazitangaza timu hizo.
Mwakalebela ameongeza kuwa wamefurahishwa kama shirikisho kwa wadhamini hao kuendelea kudhamini Mashindano hayo kwani yanaleta msisimko kwa vilabu vyetu kuweza kujitangaza Nje ya nchi.
Naye Meneja Masoko ambae pia ni wadhamini wakuu wa Mashindano hayo George lyaruu amezitaja zawadi za washindi ambapo kwa mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shiringi milioni 40 wakati mshindi wa pili atapata milioni 20 n a mshindi wa tatu ataondoka na Milioni 10.
Lyaruu ameongeza kuwa Timu itakayon'gala kwa kuwa na nidhamu bora kuliko timu nyingine itazawadiwa shilingi milioni 2 wakati Mfungaji bora wa Mashindano ya mwaka huu atatunukiwa shilingi milioni 2.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment