MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Big Brother, Elizabeth Gupta, amesema kuwa kila kitu mtu akitaka kufanya kwa ajili ya mafanikio, anaweza kutimiza malengo yake.
Akizungumza Dar es Salaam, Elizabeth alisema kuwa licha ya kutoka katika jumba hilo nchini Afrika Kusini, bado ataonekana kuwa mmoja wa wanawake waliofanya vizuri katika mashindano hayo lakini bahati haikuwa yake.
Alisema kuwa ametoka katika jumba hilo ikiwa ni siku 63 tangu aingie, lakini amejitahidi kadri ya uwezo wake na anatarajia kufanya vizuri zaidi katika miaka ijayo.
"Nafurahi sana kurudi nyumbani salama, nimeweza kufanya vizuri kadri ya uwezo wangu hivyo natarajia kufanya vizuri zaidi katika miaka ya karibuni, hata kama sijabahatika kuwa mshindi wa kwanza katika jumba la Big Brother, bado mie najiona mshindi" alisema Elizabeth.
Alisema kuwa anatarajia kutafuta chuo kwa ajili ya kujiendeleza katika sanaa na hivyo anaahidi kufanya mabadiliko makubwa katika medani hiyo.
Elizabeth aliwasili nchini jana usiku akitokea Afrika Kusini baada ya kutolewa katika jumba la Big Brother.
No comments :
Post a Comment