Kocha mkuu wa klabu ya kikapu ya Memphis Grizzlies Drew Graham akimtibu mchezaji wa kati wa klabu hiyo Hasheem Thabeet wakati wa kota ya kwanza ya mchezo wa jana wa NBA dhidi ya Portland Trail Blazers.
Mchezaji wa kati wa timu ya Memphis Grizzlies Hasheem Thabeet amevunjika taya lake la chini siku ya jana, alipokuwa akichezea na timu yake wakiminyana na Portland Trail Blazers, mchezo amabo ulimalizika kwa Blazers kutoka na ushindi wa pointi 93 kwa 79.Hii sasa inamaanisha kuwa Hasheem hatokuwemo kwenye msafara wa timu yake ya Grizzlies itakapokuwa ikienda kucheza na Houston Rockets usiku wa leo.
Hata hivyo habari si mbaya sana za kuumia kwake kwani baada ya uchunguzi wa madaktari imefahamika kuwa, hatohitaji upasuaji, ili kutibu maumivu na wakasema anatarajiwa awe amepona si muda mrefu sana kuanzia sasa, na ni wazi kuwa hii ni taarifa njema ambayo Thabeet atakuwa amefurahishwa nayo, timu yake na Watanzania kwa ujumla.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment