Simba hadi sasa inaongoza msimamo wa kundi ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 30 katika michezo kumi iliyocheza, ikiwa na rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Wakati huo huo BENDI ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma (Msondo(Music Band) inatarajia kufanya shoo kubwa ya kuitambulisha albamu yao mpya itakayotambulika kwa jina la 'huna Shukrani' tarehe 27 mwezi huu kabla ya uzinduzi wake utakaofanyika mapema mwaka huu.
Utambulisho wa albamu hiyo utakwenda sambamba na utambulisho wa wanamziki wapya wa bendi hiyo walioingia hivi karibuni Edo Sanga na Rashidi Mwizingwe.
Akizungumza Dar es Salaam,Meneja wa bendi hiyo Said kiberiti alisema oneshoo hilo litakuwa maalumu kwa ajiri ya kuwaweka sasa wapenzi wa bendi hiyo ili waweze kuipokea albamu hiyo mpya yenye nyimbo saba.
Alisema kutokana na kuwa kimya kwa mda mrefu mashabiki wao watakuwa wamekata tamaa kwa hiyo wameadaliwa shoo hiyo ili waweze kuburudika nao kabla ya uzinduzi wake.
''Tumeadaa onyesho maalumu litakalofanyika hapa Dar es Salaam katika ukumbi utakaotajwa baadaye ili mashabiki wetu waamke wasifikiri kama tumewaacha na pia siku hiyo tutawatambulisha tena wasanii wetu ambao tumewapokea mwaka huu,'' alisema Kiberiti.
Alizitaja nyimbo zitakazokuwa katika albamu yao ni Huna shukrani ulioimbwa na (Saidi mabela),cheo ni Dhamana(Edo sanga),Kiapo(hussein Jumbe),Mama kosi(Joseph Mahina)Haki yangu iko wapi(Huruka Huvuruge),Kimya kingi(Dj Papa) pamoja na Albino ulioimbwa na wanamziki wote wa bendi hiyo.
Kiberiti alisema pia kutakuwa na kikundi kingine kitakachosindikiza onesho hilo ambacho kinaandaliwa na kitatangazwa kwa wapenzi kabla ya oneshoo kufanyika.
Mbali na maandalizi ya albamu yao hiyo Kiberiti alifafanua kuwa bendi hiyo imeanza maandalizi ya utunzi wa nyimbo mpya ambazo zitakuwa maalumu kwa ajili ya mwaka ujao wakiwa na lengo la kuendeleza burudani kwa mashabiki wao.
No comments :
Post a Comment