
Raisi Mwai Kibaki akizungumza katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta amesema ujio wa kombe hilo ni tukio la kihistoria nchini Kenya na nichangamoto kwa taifa hilo katika kuendeleza michezo.

Amesema kuwa Kenya ina miundo mbinu bora yakuweza kuwasilianan na pande zote za Dunia ni ni masaa machache kwa Ndege kwenda Afrika Kusini.
Raisi Kibaki amesema kufanyika kwa kombe la Dunia kwa mara ya kwanza barani Afrika 2010 kutaifanya Kenya kupata nafasi ya kufaidika kwa Timu nyingi na mashabiki wengi wa Soka watakaopita kwenda Afrika Kusini.
Safari ya kombe la FIFA la Dunia inadhaminiwa na Coca-Cola.
Safari ya Kombe la Dunia ni ya siku 70 katika mataifa 52 ya Africa litaishia Afrika Kusini Desemba 3 huku mataifa 32 yatashirika fainali zijazo za kombe la Dunia.
No comments :
Post a Comment