Ni nani atakayeibuka mbabe katika pambano la ngumi la uzito wa juu duniani kuwania mkanda wa WBA kati ya Nikolay Valuev wa Russia na David Haye? Jibu la swali hilo litapatikana usiku wa kesho mjini Nuremberg , Ujerumani.
Bingwa mtetezi wa mkanda wa WBA, Valuev Jumamosi ataoneshana kazi kwa raundi 12 na Haye ambaye anawania ubingwa wa Dunia wa uzito wa juu Duniani kwa mara ya kwanza baada ya kupanda kutoka uzani wa cruiser .
Valuev atapanda ulingono huku akiwa na faida ya urefu na uzito mkubwa dhidi ya mpinzani kwa Haye ambaye amesema kuwa hatishiki na umbo, urefu pamoja na suara mbaya ya mpinzani wake kwenye mwili wenye vinyweleo vingi.
Mabondia hao walikutana uso kwa uso mjini Nuremberg katika mkutano wa kuhamasisha pambano hilo ambapo kila mmoja alitamba, huku Valuev akisema kuwa hana maneno mengi, ni ngumi zitazungumza.Haye amesema kuwa mpinzani wake anazidi kuongezeka siku hadi siku ikiwemo kichwa chake na kusema kua anakusudia kumtwanga, katika pambano hilo kitu ambacho kitamfanya asiuombe kupigana naye tena.
Katika mkutano huo Valuev, hakusema maneno mengi. Mapromota wake ndito walionekana kuguswa na maneno hayo kuliko mwenyewe.
“ NInaamini mitamtwanga kwa ko,” Haye alitamba katika mkutanouliofanyika Arena Nurnberger Versicherung.
“Nitakwenda ubingwa nyumbani," alisema haye huku akisema kuwa maandalizi yake yalikwua magumu sana kwa ajili ya pambano hilo muhimu zaidi katika maisha yake.
Amesema ilikuwa ngumu kuwapata wakufunzi warefu kama mpinzani wake wakati wa maandalizi. Kasema kuwa pambano hilo litakuwa kama la Daudi na Goliath .na kutamba kua yeye ana kazi zaidi kuliko mpinzani wake, hivyo anaamini kuwa atashinda.”
Mpinzani wake Valuev amesema. “Ingawa sijapigana kwa muda, sikukaa tu na kubweteka,... NIlianza maandaliazi kuanzia mwishoni mwa juni. Katika wiki chache zilizopita nilikuwa nikijiandaa rasmi kwa ajili ya
David Haye. Ni mpinzani imara lakini hatanipiga mimi.”
Valuev ana rekodi ya kucheza mapambano 50, kupoteza moja ameshinda 34 kwa Ko ana uzito wa kilo 147 urefu wa futi saba na nchi mbili.
Haye amecheza mechi 22 amepoteza moka na kushinda 21 kwa Ko ana urefu wa futi sita na inchi 3 huku akiwa na uzito wa kilo 95.555.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment