Ungozi wa chama cha Wushu Tanzania wanatarajia kuzindua chama hicho mwanzoni mwa February
mwakani ili kujulisha wachezaji na wapenzi kutambua kuwepo kwa chama hicho.
Akizungumza na kipindi cha michezo cha Radio Times FM Rais wa Mchezo huo hapa nchini Mwarami Shaweji Mitete amesema kwa muda mrefu walifanya jitihada za kusajili chama hicho ndipo mwezi Agost mwaka huu na uzinduzi huo utakuwa kama changamoto ya kukutana na wachezaji mbalimbali na kupanga mikakati ya pamoja.
Amesema kwasasa chama hicho kinaendeshwa bila kuwa na fedha za kutosha kutokana na viongozi kukosa fedha kwa wadhamini mbalimbali.Hata hivyo Wachezaji watano waliondoka wiki iliyopita nchini China kushiriki mafunzo ya mwaka mmoja wamefika salama isipokuwa wana matatizo ya kiafya inayosababishwa na hali ya hewa.
Wachezaji hao ni Omary Upinde, Ramadhani Maneno, wachezaji wawili kutoka katika kundi la mama Afrika, na wawili kutoka katika kundi la Bagamoyo.
Wushu ni mjumuiko wa michezo ya kichina inayochezwa na sakarakasi, Kungfuu, Taichii na Tajakwan.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment