Jumla ya shilingi milioni mia nne ishirini laki mbili na thelathini na tano elfu 420,235,000 zimepatikana katika mchezo uliochezwa Octoba 31 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kati ya Yanga na Simba.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa TFF Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania Fredrick Mwakalebela amesema katika mtanange huo uwanja ulikusanya watu arobaini na nane elfu laki sita na na themanini na saba elfu 48,687.
Mwakalebela ameongeza kuwa Tiketi za madaraja matatu ziuliuuzwa zote ambazo ni 5000,7000, na 10,000. lakini kwa tiketi za VIP A, B na C mkabala na jukwaa kuu kwa tiketi za elfu ishirini ziliuuzwa chache.
Wakati huo huo Mwakalebela amevukumbusha Vilabu vyote vinavyoshiriki Ligi kuu Tanzania bara kuwa kipindi kifupi cha usajili cha msimu wa 2009 -2010 kuwa kimeaanza Novemba 1 kama ilivyoainishwa kwenye kalenda ya Tff.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment