WAZIRI wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika anatarajiwa kuiwakilisha Serikali wakati kombe halisi la Dunia litakapowasili leo kwenye uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa katika ziara ya kuzitembelea kila nchi ya Bara la Afrika chini ya udhamini wa kampuni ya CocaCola.

Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja Masoko wa kamuni ya Coca Cola Tanzania Rita Tseai alisema kampuni hiyo imejiandaa kuchangamsha mapokezi hayo ambayo yatapambwa na burudani mbalimbali kwa ajili ya kuongeza hamasa kwa wapenzi wa mchezo wa soka.
"Kutokana na hamasa inayotaokna na kombe hili ambayo ni nembio kuu ya soka Dunia, Coca Cola inafanya kazi kwa karibu na maafisa wa uwsanja wa ndegewa Mwalimu Nyerere na wahusika wengine kuhakikisha uwsalama unakuwepo na kuifanikisha ziara hii kwa ujumla", alisema.
Alisema likiwa nchini maelfu ya mashabiki wanatarajia kujitokeza kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na viwanja vya Forodhani, Zanzibar kuliona kombe hilo na kupiga nalo picha ambapo pia aliongeza kuwa watapata nafasi ya sinema maalumu ambayo itakuwa ikionyesha matukio kadhaa muhimu ya kukumbukwa ya kombe la Dunia la FIFA na burudani nyingine nyingi.
"Baada ya kuwasili kombe hilo siku ya itakayofuata (ijumaa) litakuwa hapa uwanja wa Taifa kwa ajili ya mashabiki wa soka kuja kuliona na kupiga nalo picha ambapo kwa upande wa uwanjani mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali", alisema
Alisema sehemu ya kwanza ya ziara ya kombe hilo itafika kilele Desemba 3 mwaka huu huko Cape Town , Afrika Kusini ambapo ratiba ya mwisho ya fainali za kombe la Dunia za mwaka 2010 itapangwa kwa tena kwa mara ya pili mwezi januari kwa ajili ya katika nchi kadhaa duniani ambapo itafikia kilele chake mwezi Aprili mwakani.
Alisema ya kombe hilo kwa mwaka huu ni ndefu zaidi duniani ambapo FIFA ikishirikian na kampuni ya Coca Cola italitembeza kombe hilo halisi katika mataifa 86 ziara ambayo itachukua siku 225.
No comments :
Post a Comment