Na Florian Kaijage
Cairo, Misri
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo amesema kipigo cha mabao 5-1 ilichokipata timu yake juzi Alhamis usiku kutoka kwa Misri kimeipa funzo kubwa timu yake juu ya namna ya kucheza na timu za kiwango cha juu kama Misri
Kocha Maximo ambaye hiyo ni mara ya kwanza kwa timu yake kufungwa idadi kubwa zaidi ya magoli alisema motekeo hayo ni mabaya lakini jambo kubwa kwake ni kwamba ameona mchezo umempa changamotyo na maeneo ya kujifunza.‘ Timu yetu haikucheza vema katika dakika za mwanzo, wenyeji walipata magoli ya mapema na hivyo kuwachanganya wachezaji wangu ambao kiuzoefu hawalingani kabisa na wa Misri, ilikuwa ni hali ngumu kwa jumla’
Akaongeza ‘Misri ni timu ya kiwango cha juu sana, tumekuwa tukijitahidi kupata michezo ya namna hii ili kujipima uwezo wetu na hivyo kuweza kupiga hatua kwa kucheza na wale waliotuzidi, tukitaka kusonga mbele lazima tukubaliane na changamoto za aina hii’.
‘Walikuwa mbele ya mashabiki wao waliokuwa wakiwashangilia kwa nguvu, waliuanza mchezo kwa kasi ya ajabu na malengo yao yakafikiwa, lazima tupunguze amkosa katika michezo ya namna hii’ alisema Maximo huku akiutaja mchezo huo kuwa ndiyo mgumu zaidi kuwahi kukabiliana nao tangu aanze kibarua cha kuinoa Stars Agosti 2006.
Katika mchezo huo ulipigwa Kusini mwa Misri katika mji wa Aswan na kuhudhudriwa na mashabiki wapatao 12,000, Taifa Stars ilijikuta iko nyuma baada ya dakika 9 tu pale Emad Metab alipofunga kwa kichwa kufuatia kros ya mlinzi Hany Said. Dakika nane baadaye Misri walikuwa mbele kwa magoi mawili baada ya mshambuliaji hatari Amri Zaki kupiga kiufundi mpira wa juu ulimshinda mlinda lago Ali Mustapha. Kufikia dakika ya 33 Taifa Stars ilikuwa tayari iko nyuma kwa magoli 3-0 baada ya Metab kufunga bao lake la pili kwa mkwaju mkali wa kimo cha kadri.
Dakika tatu kabla ya mapumziko wamisri waligongeana mipira kwa kasi ya ajabu kati ya Zaki Metab na kiungo Ahmed Hassan kabla ya kumgongea mzoefu Mohamed Barkat aliyeachia mkwaju mkali wa chinichini na kuujaza kimiani.
Baada ya hapo Misri walianza kupunguza kasi ya mchezo na ndipo Kigi Makasi aliyeingia kuchukua nafasi ya Mussa Hassan Mgosi alipomtungua mmoja wa walinda lango bora kabisa Afrka, Esam Elhadery kwa kombora kali la umbali wa mita 30 na hivyo kuipesha Stars na kipigo kikubwa zaidi chini ya Maximo tangu ifungwe 4-0 na Senegal March 24, 2007.
Kigi alikuwa ni mchezji wa pili kumbadili mchezaji mwenzake akitanguliwa na Abdulahim Humoud aliyechukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto baadaya dakika 27 tu.
Uchezaji bora zaidi na kufuata maelekezo katika kipindi cha pili ni jambo amabalo,limemfurahisha zaidi kocha Maximo.
‘Kipindi cha pili timu ilitulia, lakini ilianza kutulia zaidi baada ya dakika 30, japo wakati huo tayari tulikuwa tumefungwa magoli ambayo kwa kipimo chochote yalikuwa ni mengi, tulirejea katika mchezo wetu na wakati fulani tuliwabana sehemu ya kiungo na kukaribia kupata magoli, alieleza mtaalamu huyo kutoka Brazil.
Katika kipindi cha kwanza Taifa Stars ilipiga mashuti mawili tu golini moja la Kigi lililozaa goli na lingine ni la Mrisho Ngasa katika dakika ya 29 pale mpira aliotaka kuuvusha juu ya Elhadery ulimgonga mlinda lango huyo usoni na kutoka nje.
Hata hvyo katika kipindi cha pili Stars ilifanya mashambulizi mengi zaidi na kupiga mashutu ambayo yaliiwezesha kupata kona 8 ambazo hazikuzaa matunda. Katika kipindi cha kwanza Stars haikupata kona hata moja.
Kuhusu mlinda lango Ali Mustapha ambaye alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Shaban Dihile mwanzoni mwa kipindi cha pili, kocha Maximo aliamua kumpatia nafasi kutoka na kujituma mazoezini.
Pia alisema katika magoli manne aliyofungwa ni goli la pili pekee lililofungwa na Zaki ambalo anaweza kusema ni makosa ya Mustapha kwani alikuwa amasogea mbele kidogo ya lango lakini akasema mfungaji wa goli (Amri Zaky) ni mchezaji wa kiwango cha juu mno na anafahamu namna ya kutumia makosa madogomadogo ya timu pinzani. Zaky alikuwa akichezea klabu ya Ligi Kuu ya England, Wigan kwa mkopo kabla ya kurejea hapa Misri kukipiga katikaklbau yake ya Zamalek.
Taifa Stars inaondoka asubuhi hii (Jumamosi) kuelekea Yemen ambao itacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo. Mchezo wa kwanza utachezwa kesho Jumpili na mwingine utachezwa Jumatano ijayo Novemba 11.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment