Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka hapa Nchini TFF Sunday Kayuni amesema Watanzania tunatakiwa tuamke kwa kuanza kufanya mipango mapema ili kuhakikisha tunachukua Kombe la Dunia badala ya kuwa watazamaji.
Kayuni ameyasema hayo hii leo katika kumbi wa TFF wakati wakiwa na Wadhamini wakuu wa Kombe hilo la Dunia Kampuni ya kinywaji cha Coca cola na watengenezaji wa Magari aina ya Hyundai, Kayuni amesema hii ni mara ya pili kwa Kombe hilo kuja hapa nchini hivyo hii ni changamoto kwetu sisi kuanza kujipanga.
Naye Afisa mwandamizi wa masoko wa Kampuni ya Hyundai Antony Nyeupe amesema katika ujio huo wa Kombe hilo watahakikisha suala zima la usafiri wa ardhini unapatikana kwa kipindi chote, kwa kutoa magari kumi kama moja ya makubaliano wa mkataba wao.
No comments :
Post a Comment