Klabu ya Simba imesema haiamini wachezaji wake wawili Danny Mrwanda na Emmanuel Okwi wanaweza kufanya kitendo cha utovu wa nidhamu katika mchezo wake dhidi ya mtani wake wajadi Yanga uliochezwa Octoba 31 mwaka huu.
Afisa Habari wa Simba Sports Klabu, Cliford Mario Dimbo amesema taarifa zinazoenea kuhusiana na wachezaji hao si za kweli na wanasubiri ripoti ya Kamisaa itasema nini.
Ndimbo ameongeza kuwa wameshawazoea Klabu ya Yanga kuwafuatafuata kwa vitu ambavyo hawavijui hivyo kuwataka wasubiri utaratibu wa TFF utakavyosema.
Aidha Ndimbo amesema katika kipindi hiki ambacho wanasubiri wachezaji wao warejee toka Misri walipokwenda na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, wanataraji kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Azam FC.
Akizungumzia kuhusu Usajili wa Timu hiyo ambapo kwa sasa kalenda ya TFF inavyoonyesha kuwa kipindi hiki ni cha usajili kwa Vilabu vyote vinavyoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara, Ndimbo amesema Benchi la ufundi chini ya Kocha Patrick Phiri ndilo litaamua lakini msimu uliopita walisajili Wahezaji 28 hivyo anaamini wataongeza wachezaji wawili 2 ili kutimiza wachezaji 30 na hawana mpango wa kumuacha mchezaji yoyote .
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment