WASHIRIKI wanaowania umalkia wa Kisura wa Tanzania, tayari wameingia kambini katika hoteli ya Kiromo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Akizungumza hotelini hapo, Meneja Mradi wa kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency, Grace Kilembe, washiriki hao walipatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.
Aliitaja mikoa iliyofanyiwa usaili na kuwapata washiriki hao walioingia kambini juzi ni Singida, Dodoma, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Arusha, Mara na Dar es Salaam ambapo waliwapata wasichana 20 wenye vigezo vya mashindano hayo.
Aliwataja wasichana hao na mikoa waliyotoka kwenye mabano ni Mwajabu Juma (Mwanza), Lucky Mwakatobe, Resson Soto (Arusha), Jack's Oyombe, Alinda Lema, Violety Mganga, Sharon Silas (Dar es Salaam), Jackline Benson (Arusha) na Gloria Gilbert (Tanga).
Wengine ni Glady Molel, Lightness Mwanga, Mwatatu Francis, Mary Joel, Shamim Babu (Manyara) na Mary Mallya (Dodoma), Asnat Mohammed na Diana Ibrahim (Mara).
Alisema washiriki hao watakaa katika kambi kwa muda wa mwezi mmoja na wiki mbili huku wakitoka mmoja mmoja mpaka watakapobaki 10 ambao wataingia fainali ya mashindano hayo.Grace alisema visura 10 watakaoingia fainali hiyo watapatikana kwa njia ya kupigiwa kura na watazamaji wa televisheni ya TBC1.
Mashindano ya Kisura wa Tanzania yamedhaminiwa na Serengeti Breweries Limited (SBL), Kiromo Resort, TBC1, Clouds FM, FHI, ATC, Entertainment Masters, Mwananchi Communication, Hugo Domino, Mercy G Parlor Beauty na Bang Magazine.
Grace alisema mwaka huu walijitokeza visura wengi katika hatua za awali tofauti na mwaka jana na kuwapa moyo waandaaji hao kuwa, wengi wameanza kuyaelewa mashindano hayo na manufaa yake.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment