KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zanziba Telecom Ltd (Zantel) imezindua huduma mpya ijulikanavyo kama Tsh 1 + Sms za bure inayowapa wateja wa mtandao huo malipo kabla ya wanaotumia viwango hivyo kwa sekunde.
Akizindua huduma hiyo Dar es Salaam kwa waandishi wa habari,Mkuu wa Mauzo Bw.John Mbaga amesema kuwa Zantel imeamua kuzindua huduma hiyo kwa wateja wake ili kutimiza ahadi zake walizoahidi awali na kuwapa fursa za kuendelea kutimia mtandao huo.
Bw.Mbaga amesema kuwa mpango huo utaendelea kuwawezesha wateja wake kuongea zaidi na kujipatia Sms za bure zitakazowawezesha kuwasiliana na ndugu,jamaa na marafiki kwa muda wa mchana na usiku.
Amesema kuwa kampuni ya Zantel imejitolea kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora kwa watanzania kwa bei nafuu na inaamini kuwa mtandao huo ndio wa kwanza na wa kipekee Tanzania kutoa sms za bure.
No comments :
Post a Comment