
Mmoja wa Waamuzi hao akizungumza na kipindi cha michezo na burudani wametanabaisha kuwa mara kwa mara wanapuulizia kuhusu posho zao wanaambiwa kuwa wasubiri huku wengine wakiambiwa kuwa tayari wameshalipwa.
Waamuzi hao wamesema wamekuwa wakitupiwa lawama na tuhuma za rushwa katika michezo ya ligi kuu na kupelekea wenzao kufungiwa lakini wamedai TFF inachangia waamuzi hao kupokea rushwa kufuatia kutolipwa posho zao kwa wakati.
Amesema unakuta mwamuzi anatumia fedha zake za mfukoni hadi zinakwisha bila kupatiwa posho ilihali wanasafiri na kulala gesti, na kuhoji vipi wanaweza kujikimu.
Wamesema kuna baadhi ya waamuzi tangu michuano ya ligi daraja la kwanzaimeanza hawajapatiwa fedha zao achilia mbali ambao hawajalipwa malipo ya michezo mitatu, hadi mitano.
No comments :
Post a Comment