Meneja wa Bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah (kulia) akimkabidhi tuzo pamoja na cheti mchezaji wa mchezo wa pool, Godfrey Mhando, wakati wa hafla ya makabidhiano ya vyeti kwa wachezaji waliyoshiriki mashindano ya Afrika yaliyofanyika Afrika Kusini, anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa PoolTable Tanzania (TAPA), Isack Togocho.(Picha na Rajabu Mhamila)
TIMU ya mchezo wa Pool Tanzania wanatarajia kushiriki mashindano ya Dunia ya mchezo huo yaliyopangwa kufanyika nchini Ufaransa kuanzia Novemba 6 hadi 13 mwakani.
Timu hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yke ya Safari, ilipata nafasi hiyo baada ya kushika nafasi ya tano katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Afrika Kusini.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Safari, Fimbo Butalah alisema kutokana na mafanikio hayo wanatarajia kuongeza thamani ya mashindano ya ndani ambayo ndio yanayotoa timu ya Taifa.
Amesema kwa kuwa matunda ya timu hiyo yametokana na mashindano ya Taifa ya mchezo huo hivyo katika harakati za kuboresha mchezo huo wanatarajia kuongeza thamani ya mchezo huo kupitia mashindano hayo.
Alisema mbali na kupata nafasi hiyo lakini pia timu hiyo ambayo iliwakilishwa na wachezaji watano walipata mafanikio ya mchezaji wake Godfrey Mhando kuchaguliwa katika timu ya wachezaji watano bora wa Afrika.
Fimbo amesema kuwa mchezaji Omary Akida ambaye mwaka jana alikuwa katika timu ya Afrika mwaka huu amefanikiwa kuingia hatua ya robvo fainali ya michuano hiyo kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Pool Tanzania (TAPA), Isaack Togocho alisema mafanikio hayo ni changamoto kwa timu yao na mafanikio hayo yametokana na mwalimu kutoka Zambia ambaye alikaa na timu kwa kipindi kifupi na wanatarajia kuwa naye ili kuiboresha zaidi timu hiyo kabla ya kwenda katika mashindano hayo ya Dunia.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment