
Cannavaro amesema leo ni siku ya sita tangu afike kutoka Cannada hivyo alichelewa kujiunga na kambi hiyo hivyo majina yalipelekwa mapema walidhani kuwa hatoweza kufika hapa nchini lakini wachezaji waliokwenda ni 19
Aidha Cannavaro amekanusha madai ya kutaka kujiunga na simba na kudai hana mpango wa kujiunga na klabu yoyoye hapa Nchini kwani bado anamkataba na Timu ya Yanga wa miaka miwili na anaipenda Timu hiyo.
Nadir Haroub Cannavaro amerejea kutoka nchini Canada alipokuwa akiichezea timu ya Vancouver Whitecaps kwa kipindi cha miezi mitatu hivyo mkataba wake umekwisha na kuamua kurudi nyumbani kuendelea kuichezea klabu ya Yanga.
No comments :
Post a Comment