Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, November 21, 2009

ISAKA STEPHANO MISS UTALII TANGA

Iska Stepahano jana alitangazwa mshindi wa Fainal za Miss Utalii Mkoa wa Tanga baada ya kuwashinda wenzake 9 katika kinyang’anyiro kilichofanyika katika Ukumbi wa Beach Resort kandokando ya Bahari ya Hindi ambapo mgeni Rasmi alikuwa ni Wilaya ya Mkinga, Kinawilo Edward aliyemvisha taji baada ya kutangazwa Mshindi.Katika fainal hizo ambazo zilitikisa mkoa wa Tanga, jumla ya washiriki kumi walipanda jukwaani katika mavazi mbalimbali ambayo yalibunia na mbunifu wa mavazi wa kimataifa hapa nchini, Fatma Amour, ambaye aliingia hapa hivi karibuni akitokea nchioni Marekani ambako alikuwa katika mwaliko wa kuonyesha mavazi na kujifunza masuala ya Usanii.Warembo hao wakiwa katika mavazi ya aina tofauti yakiwemo ya Utamaduni wa Tanzaniana Asili ya Kiafrika, ambapo Vikundi mbalimbali vya Muziki vilitumbuiza akiwamo Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Dansi Mwinjuma Mumin, mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Maunda Zoro,na Kassim Mganga
Katika shindano hilo mshindi wa kwanza alipata kitita cha shilingi laki tano taslim, wa pili laki moja na nusu, wa tatu laki moja , wa nne laki moja na wa tano kiasi cha shilingi laki moja, wakati barozi wa Tanga Beach Resort ambaye pia ni Miss Utalii Tanga 2009- Iska Stephano alikabidhiwa TV yenye thamani ya shilingi laki 4, huku washiriki wengine wakipata kifuta jasho cha shilingi helfu hamsini kila mmoja.
aidha katika shindano hilo Mbunifu wa Mavazi wa Kimataifa Fatma Amour, alimvisha Taji, la kiasili lililotengenezwa kwa Ustadi Mkuu ambao uligharimu kiasi cha shilingi laki moja na Nusu, likiwa na Alama ya Bendera ya Taifa.Warembo walioshiriki Fainal hizo ni pamoja na Iska Stephano, Lyna Lucas, Judith Assey, Vaileth Michael, Imakulata Njuu, Ashura Nasri, Ummy Ally, Grece Joseph, Mariam Rajabu, na Fuse Kilenge Asile, ambapo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ni pamoja na IIska Stephano, Lyna Lucas, Vaileth Michael, Judith Assey na Grece Josephat.Washindi watano katika fainal hizo watashiriki katika hatua ya Kanda ya Mashariki ambayo inajumuisha mikoa ya Dar es Salaa, Morogoro, Pwani, Mtwara, na lindi,

No comments :

Post a Comment