Kampuni ya Coca Cola Tanzania Leo imezindua rasmi kipindi cha Luninga cha michuano ya Copa Coca Cola (Copa Coca Cola Reality Show) ambacho kinaelezea wasifu wa wachezaji toka nchi nane za Afrika akiwemo Mtanzania Murshid Alley.
Kipindi hicho kinalenga zaidi kkuelezea mafanikio ya michuano ya Copa Coca Cola ya mwaka 2009.
Kipindi hicho cha Luninga kitaonyesha mafanikio ya mashindano hayo yaliyofanyika kati ya Februari na Julai mwaka huu, pia kitaonyesha wasifu wa wachezaji kutoka Ethiopia ( Ermias daniel), Zambia ( Isaac Chongo) Zimbambwe (Samson Nyamunda), Namibia (Leighton Wemment), Kenya (Ian Otieno) Uganda Isaac Owori na Afrika Kusini (Pule Letshaba).
Mashindano hayo yalifanyika Juni Mwaka huu huko Afrika Kusini yakijumuisha vijana wenye umri chini ya miaka 17.
wakati huo huoZikiwa zimesalia siku 15 kabla ya kombe la Dunia halijatua nchini Tanzania katika ziara kwa nchi za Afrika shirikisho la kandanda Tanzania limesema tayari limekwishaanza kukutana na viongozi wa serikali kuweka maandalizi mazuri ikiwa ni pamoja na kudumisha muungano.
Katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela ameyasema hay oleo katika mkutano na waandishi wa habari akisema tayari wamekwishaunda kamati mbali mbali pamoja na kukutana na viongozi wa chama cha soka Zanzibar.
Naye Meneja Masoko wa Coca Cola Afrika Mashariki na Kati Rita Tsehai amesema wamefanya kazi kubwa kuwashawishi kombe hilo kwenda Zanzibar kwani ratiba tayari ilikwisha pangwa tangu mwezi Desemba mwaka jana.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment