Timu ya taifa kesho inatupa karata yake ya tatu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Yemen.
Afisa Habari wa shirikisho la kandanda Tanzania TFF Florian Kaijage ambaye ameambatana na Taifa Stars nchini Yemen amesema timu imejiandaa vema kuhakikisha inalinda heshima ya Taifa katika mchezo huo ambao ni wa pili.
akizungumza nami kwa njia ya simu nimemuuliza, moja kwa moja toka Yemen amesema hali ya wachezaji ni nzuri na wamaefanya mazoezi jana na leo.
Kaijage amesema ni Mrisho Ngasa pekee ndiye aliyekuwa akisumbuliwa na Malaria lakini kwa sasa hali yake ni nzuri na leo amefanya mazoezi.
Amesema katika mchezo wa Kesho Taifa Stars inauhakika wakuibuka na ushindi dhidi ya Yemen katika mchezo wa pili wa kirafiki.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment