Akizungumza na kipindi cha michezo na burudani Msemaji wa Afrikan Lyon Hassan Mvula amesema wanaufahamu uwezo wa Mkwassa na ndiye atakayeliokoa jahazi hilo lisizame.
Mvulla amesema wanaamini uzoefu wa ligi ya soka Tanzania aliyonao Mkwassa pamoja na uzoefu wake katika timu ya taifa ya wanawake utaisaidia klabu hiyo kuhakikisha wanabaki ligi kuu.
Naye Kocha Boniface Mkwassa amesema atafanya jitihada za maksudi ili kuhakikisha mzunguko wa ligi kuu unamalizika na timu ya Afrikan Lyon inabaki katika nafasi yake.
Amekiri anajukumu la kuifundisha timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania ambayo inajiandaa na michuano ya nchi za Magharibi mwa Afrika, lakini endapo atapatikana mtu mwingine wa kuifundisha timu ya taifa ya wanawake yuko tayari kuachia ngazi.
Amesema licha ya mapenzi yake katika kufundisha soka la wanaume, lakini michezo hivi sasa ni ajira hivyo swala la maslahi ni muhimu kwa mwanamichezo yeyote, hivyo naye amekwenda African Lyon kufuata donge nono la fedha.
No comments :
Post a Comment