Vancouver Whitecaps FC imetangaza kuwaongezea mkataba wachezaji wa tatu akiwemo Mlinzi na kiungo Takashi Hirano, pamoja viungo Justin Moose na Nizar Khalfan.
wachezaji wote wa tatu wamesaini mkataba wa mwaka mmoja. Pia klabu ya Whitecaps hawatowaongezea mkataba wachezaji wawili Chris Pozniak na Nadir Haroub Ali.
Hirano, mwenye umri wa miaka 35, amerejea katika klabu hiyo kwa msimu wa tatu baada ya kupata mafanikio katika miwili ya kwanza akiwa na Vancouver. mchezaji huyu anacheza nafasi ya ulinzi wa kushoto katika kikosi cha kocha Teitur Thordarson.
Mchezaji huyo ambaye ni mkazi wa Shimizu City, Japan, amejitokeza mara 38 akiwa na klabu hiyo akiwa na jumla ya dakika 3,248 uwanjani katika msimu wa 2009.
Dakika nyingi za Hirano ni ishara tosha kuwa ni moja ya wachezaji waliyofanya vizuri katika klabu ya Whitecaps. mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Japan amejitokeza katika michezo 68 katika kipindi cha misimu miwli.
Moose, mwenye umri wa miaka 25, naye pia amesaini mkataba huu ikiwa ni msimu wake wa tatu akiwa na Whitecaps licha ya kukabiliwa na majeraha katika kampeni 2009. Mchezaji huyu anatokea Statesville, North Carolina, amejitokeza katika michezo 15 huku akicheza dakika 484, aliwahi kucheza kama mshambuliaji wa pembeni katika msimu wake wa kwanza akiwa na Vancouver.
Nizar Khalfan, mwenye umri wa miaka 21, sasa atacheza msimu wake wa kwanza akiwa na Whitecaps katika msimu wa 2010 baada ya kujiunga na Vancouver akitokea katika ligi kuu ya Tanzania ambapo alikuwa akiicheza klabu ya Moro United kwa mkataba huru tangu mwezi August 13.
Nizar Khalfani kwa sasa anacheza katikati ama kiungo wa kulia.
Nizar Khalfani ni mwenyeji wa Mtwara, Tanzania, ameanza katika michezo 14 akiwa na Whitecaps huku akiwa na dakika 729 za uwanjani. Hii inajumuisha mitano aliyojitokeza huku mchezo mmoja akianza katika hatua ya mtoano mwaka huu 2009.
Pozniak, mwenye umri wa miaka 28, anaondoka Whitecaps baada ya kumaliza msimu wake wa pili akiwa na klabu hiyo. Ni mzaliwa wa North York, Ontario, amejitokeza katika michezo 14 baada ya kusaini mkataba mpya mwezi July 30.
Katika msimu wake wa kwanza na Whitecaps mwaka 2008, Mlizni huyo na kiungo alicheza michezo tisa kabla ya kujiunga na klabu ya ligi daraja la kwanza ya Scotland, Dundee FC.
Nadir Haroub Ali, mwenye umri wa miaka 26, anarejea katika klabu yake ya Tanzania Young Africans FC baada ya kumaliza muda wake wa kuichezea kwa mkopo. Nadir Haroub ni mzaliwa wa Michenzani, Zanzibar, hakufanikiwa kujitokeza katika mchezo hata mmoja akiwa na Whitecaps katika kipindi cha mkataba wake wa miezi mitatu aliyodumu na Vancouver.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment